Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, amemteua
Luteni Jenerali Venance S. Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
Tanzania.Pamoja na kuteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania
Luteni Jenerali Venance S. Mabeyo amepandishwa cheo na kuwa
Jenerali.Jenerali Venance S. Mabeyo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na
Jenerali Davis Mwamunyange ambaye amestaafu.Wakati huo huo, Mhe. Rais
Magufuli amemteua Major Jenerali James M. Mwakibolwa kuwa Mnadhimu Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.
Pamoja na
kuteuliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Major
Jenerali James M. Mwakibolwa amepandishwa cheo na kuwa Luteni Jenerali.
Luteni
Jenerali James M. Mwakibolwa anachukua nafasi iliyoachwa wazi na
Jenerali Venance S. Mabeyo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi Tanzania.
Uteuzi huu unaanza mara moja na tarehe ya kuapishwa itatangazwa baadaye.


Post a Comment