Mkuu
wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe akitoa heshima zake za
mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa
Singida SSP Peter Charles Kakamba, baada ya mwili kuagwa Mhandisi
Mtigumwe amewaongoza msafara wa waombolezaji kuelekea Mkoani Katavi,
kijiji cha Kawajese kwa ajili ya mazishi. Kamanda Kakamba amefariki
usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati
akipatiwa matibabu.(Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida)
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akitoa heshima
zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa
Singida SSP Peter Kakamba aliyefariki usiku wa kuamkia jana hospitali
ya taifa ya Muhimbili. Kakamba amefariki dunia baada ya kuugua maradhi
ya tumbo. Mwili huo umesafirishwa kwenda kijiji cha Kowajese Mkoani
Katavi kwa ajili ya mazishi.
Askari
polisi Mkoani Singida wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa
aliyekuwa Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Kakamba
aliyefariki usiku wa kuamkia jana hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Kakamba amefariki dunia baada ya kuugua maradhi ya tumbo. Mwili huo
umesafirishwa kwenda kijiji cha Kowajese Mkoani Katavi kwa ajili ya
mazishi.
Jeneza
lenye mwili wa aliyekuwa kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP
Peter Kakamba ukitolewa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya VETA
mjini hapa kwa ajili ya kuagwa na viongozi mbalimbali na wananchi
wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe.
Baada ya kuagwa kwa mwili huo umesafirishwa hadi kijiji cha Kawajese
Mkoani Katavi kwa ajili ya mazishi.
Jeneza
lenye mwili wa aliyekuwa Kamanda jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP
Peter Kakamba ukitolewa kwenye basi dogo lililobeba mwili huo kutoka
hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar-es-salaam. Mwili huo umefikishwa
kwenye nyumba aliyokuwa akiishi mjini Singida kwa ajili ya kuagwa leo
(01/12/2016).
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akiwashukuru
wananchi waliojitokeza kwa wigni kuungana na familia kwa ajili ya kuaga
mwili wa aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles
Kakamba, Dkt Lutambi amesema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa iko pamoja na wafiwa
na watashiriki mazishi kijiji cha Kowajese Mkoani wa Katavi.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Mayalla Towo akiwashukuru
wananchi, taasisi na mashirika mbalimbali walioshiriki msiba huo, Towo
amesema marehemu alikuwa kiongozi bora aliyependa kuwafundisha na
kuwaelekeza ujuzi na maarifa aliyonayo watumishi walio chini yake.
Wananchi waliojitokeza wakiaga mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba.
Na Mathias Canal
Mwili
wa Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi (SACP) EX Peter Kakamba umeagwa na wamia ya wakazi
wa Mkoa wa Singida wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Injinia Methew
Mtigumwe.
Kakamba alifariki dunia alfajiri ya tarehe 30/11/2016 katika hospital ya taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Kakamba
alizaliwa mwaka 1963 katika kijiji cha Kawajense Wilayani Mpanda, mkoa
wa Katavi. Alisoma shule ya msingi Shanwe Kawajense mwaka 1973 hadi
1980, Kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya Sekondari
Kantalamba mwaka 1981 hadi 1984 ambapo kidato cha tano na sita alisoma
katika shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro mwaka 1985 hadi 1987.
Mwaka 1992 hadi 1994 alisoma Astashahada ya Sheria katika Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam.
Marehemu
alijiunga na Jeshi la Polisi mwaka 1988 ambapo katika utumishi wake
alipandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Konstable wa Polisi (1989), Sagenti
wa Polisi (1991), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1997), Mkaguzi wa Polisi
(2003), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (2006), Mrakibu wa Polisi (2008),
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (2011), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2015)
na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (2016).
Baadhi
ya nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa Mwendesha Mashtaka wa
Polisi katika mkoa wa Iringa, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi, Afisa
mnadhimu wa Polisi katika Mikoa ya Iringa na Geita, Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Iringa na mpaka anafariki alikuwa Kamanda wa Polisi katika mkoa
wa Singida.
Kufuatia
kifo hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu anatoa pole
kwa Maofisa, Wakaguzi,Askari, ndugu, jamaa na marafiki kwa Msiba huo.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa,

Post a Comment