Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed
Janabi akipokea zawadi za pampers ambazo zitatumika kwa watoto
waliolazwa kutoka kwa Mary Mabano ambaye mwaka 2008 alifanyiwa upasuaji
na madaktari wa Taasisi hiyo na kuwekewa Valve moja ambayo inamsaidia
kupitisha damu vizuri baada ya upasuaji huo amepona na amejaliwa kupata
mtoto mmoja. Siku ya jana tarehe 28/12/2016 Mary alikuwa anatimiza umri
wa miaka 23 na aliamua kusherehekea siku hiyo na wagonjwa wa moyo.
Mary
Mabano akimlisha keki mgonjwa wa Moyo Nasra Hamis ambaye amefanyiwa
upasuaji na kuwekewa Valve ambayo inamsaidia kupitisha damu vizuri
katika moyo wake.
Madaktari
Bingwa wa Moyo, Wauguzi , wagonjwa wa Moyo, ndugu, jamaa na marafiki
wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa sherehe ya kuzaliwa kwa Mary
Mabano ambaye aliyesherehea siku hiyo na wagonjwa wa Moyo waliolazwa
katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). Wa tano kutoka kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi.
Mary
Mabano akimkabidhi Afisa Muuguzi Msaidizi ambaye pia ni msimamizi wa
wodi namba tatu (3) iliyoko Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
Rogers Kibula zawadi ya sabuni ya unga ya kufulia ambayo itatumika kwa
ajili ya usafi wakati wa sherehe yake ya kutimiza miaka 23 iliyofanyia
jana katika Taasisi hiyo. Mary alisherehekea siku yake ya kuzaliwa na
wagonjwa wa Moyo kwa kuwa hata yeye mwaka 2008 alifanyiwa upasuaji wa
moyo na kuwekewa Valve moja ambayo inamsaidia kupitisha damu vizuri
baada ya upasuaji huo amepona na amejaliwa kupata mtoto mmoja.
Mary
Mabano akiwa katika picha ya pamoja na Daktari Bingwa wa Moyo ambaye
ndiye daktari anaendelea kumtibu Tulizo Shemu Sanga, baba yake mzazi
Mzee Fabian Mabano ambaye amembeba mjukuu wake mtoto wa Mary aitwaye
Faraj Khalid.
Mary
Mabano akimlisha keki Mtoto Jumanne Mndeme ambaye amelazwa katika
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo.
Picha ya keki ya Siku ya kuzaliwa Mary Mabano.
Mary
Mabano akimlisha keki Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Tulizo Shemu
Sanga ambaye ndiye daktari anaendelea kumtibu Mary. Mwaka 2008 Mary
alifanyiwa upasuaji wa moyo na kuwekewa Valve moja kwa kuwa Valve
yake ya kuzaliwa nayo ilikuwa na tatizo la kutokupitisha damu vizuri.
Mary
Mabano akikata keki wakati wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa huku
Madaktari Bingwa wa moyo, wauguzi, ndugu na jamaa wakishuhudia.
Picha na Anna Nkinda - JKCI











Post a Comment