Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi amezitaka Halmashauri zote nchini kutekeleza agizo la kuunda Kamati za Watu Wenye Ulemavu kuanzi ngazi ya Vijiji, Kata, Wilaya hadi Mkoa.
Mhe.
Possi ametoa maagizo hayo kwa nyakati tofauti wakati wa ziara yake
katika mikoa ya Mwanza na Simiyu hivi karibuni ambapo alitembelea makazi
ya watu wenye mahitaji maalum ya Bukumbi, Shule ya watu wenye mahitaji
maalum ya Mitindo na kituo cha kulelea watoto wenye ualbino cha Lamadi.
Kauli
ya Dkt. Possi imekuja kufuatia maagizo yaliyolewa na Ofisi ya Waziri
Mkuu mwezi Machi mwaka huu kwa kuziandikia Halmashauri zote kutekeleza
uundwaji wa kamati za Watu wenye Ulemavu ikiwa ni sehemu ya kutatua
changamoto wanazokabiliana nazo.
“Ni
muhimu sana kutekeleza agizo lililotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu
mwanzoni mwa mwaka huu ambalo limeeleza wazi kuundwa kwa Kamati za Watu
wenye Ulemavu na ikumbukwe kuwa, suala hii lipo kisheria na lina
miongozo yake katika utekelezaji wake”. Alisema Waziri Possi.
Waziri
Possi alisisitiza kuwa maagizo ya kuundwa kwa kamati za watu wenye
ulemavu yalitolewa na Ofisi hiyo ili kusaidia upatikanaji sahihi wa
taarifa za watu wenye ulemavu ili kupata namna bora ya kutatua
changamoto zinazowakabili.
“Ofisi
ya Waziri Mkuu ilitoa agizo hilo ili kusaidia kujua mahitaji ya watu
wenye ulemavu na kuwa na njia nzuri za utatuzi wa changamoto zao kwa
kuzingatia takwimu sahihi zitakazo toa picha halisi ya hali zao katika
nyanja zote.”Alisema Dkt.Possi
Aliongeza kuwa
Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kutoa vipaumbele kwa watu wenye
ulemavu na mahitaji maalum kwa kuwapa nafasi za ushiriki katika mipango
yote ya maendeleo ikiwemo; elimu, huduma za afya na uchumi ikiwa ni
sehemu ya kuwawezesha katika jamii.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe. Juma Sweda alimpongeza Mhe. Possi kwa juhudi za kuhakikisha
sauti za watu wenye ulemavu zinasikika katika ngazi zote kwa kuudwa kwa
kamati hizo zitazotatua na kutibu changamoto za watu wenye ulemavu.
”Nikupongeze
Mhe. Waziri kwa kutembelea Wilaya yetu na kuona umuhimu wa kuweka
msisitizo wa uundwaji wa Kamati hizi, nasi tunakuhaidi kulitekeleza hilo
kama Ofisi yako ilivyoekeza ili kufikia malengo ya Serikali katika
kuhakikisha Haki na Usawa unakuwepo kwa watu wote bila kujali hali
zao”.Alisema Mhe.Sweda.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah
Possi (wa kwanza kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya
Misungwi Mhe. Juma Sweda wakati wa ziara yake katika shule ya Mitindo
yenye kuhudumia watu wenye mahitaji maalum Jijini Mwanza.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah
Possi akizungumza jambo wakati wa ziara yake katika Shule ya wenye
mahitaji maalumu ya Mitindo Wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah
Possi akisalimiana na Mwalimu wa wasioona Bw. Mika Sholla wakati wa
ziara yake katika shule ya Mitindo Wilayani Misungwi Mwanza.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah
Possi akizungumza na baadhi ya Watendaji wa Serikali katika Ofisi ya
Kituo cha Kulelea Watu wenye mahitaji maalum cha Bukumbi Wilayani
Misungwi mkoa wa Mwanza wakati ya ziara yake.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah
Possi (katikati mwenye miwani) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
wanafunzi wa shule ya Mitindo pamoja na baadhi ya Watendaji wa Serikali
wakati wa ziara yake shuleni hapo Jijini Mwanza. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU).






Post a Comment