Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii
WIZARA
ya Viwanda na Biashara na uwekezaji,imeweka wazi kuwa itaendelea
kuhakikisha kwamba tasisi zote zinafanya mabadiliko ya utaratibu ili
kuboresha uwazi ,tija na ufanisi hili kuweza kuboresha huduma kwa
wawekezaji.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage
alipokuwa akizindua rasmi kitengo cha Huduma za mahala Pamoja katika
kituo cha uwekezaji(TIC)
“Wawekezaji
tunaowahitaji Tanzania ndio haohao wanaohitajika nchi zingine hivyo
serikali itaendelea kuboresha huduma zake kuwa za uwazi ,kasi na ufanisi
zaidi”amesema Waziri Mwijage.
Ameongeza
serikali ya awamu ya tano ipo mstari wa mbele katika kuongeza uwazi
,uwajibikaji,kupiga vita Rushwa na kubana matumizi ya serikali na
kuweka wazi kuwa hii yote itafanikiwa kama kila tasisi itawajibika kama
kituo cha uwekezaji na wadau wake katika cha huduma za mahala Pamoja.
Amemaliza
kwa kusema kituo cha uwekezaji Tanzania kina mchango mkubwa sana katika
uchumi hasa kwa upande kwa kuhakikisha nchi inapata wawekezaji katika
sekta zote ,kusaidia kuwahudumia wawekezaji hao kufuatana na sheria
hasa katika uanzishwaji na utekelezaji wa miradi.
Waziri
wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Viwanda na Biashara Profesa, Adolf Mkenda pamoja na Mwenyekiti wa bodi
ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Profesa Lucian Msambichaka wakikata
utepe kuashiria uzinduzi wa Kitengo cha Huduma za Pamoja ndani ya Kituo
cha Uwekezaji nchini, zilizofanyika leo Novemba 15, 2016 jijini Dar es
salaam.
Waziri
wa Viwanda na Biashara na uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza jambo
na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford
Tandari muda mfupi baada ya uzinduzi wa Kitengo cha Huduma za Mahala
pamoja cha TIC jijini Dar es salaam leo. Katikati ni Mwenyekiti wa bodi
ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Profesa Lucian Msambichaka
Waziri
wa Viwanda na Biashara ,Charles Mwijage, akizungumza na baadhi ya watoa
huduma katika Kitengo hicho mara baada ya uzinduzi wake.
Waziri
wa Viwanda , Biashara na uwekezaji,Charles Mwijage , akizungumza wakati
wa uzinduzi wa kituo cha huduma za Pamoja leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu
ya Wafanyakazi wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) wakiwa katika hafla
ya uzinduzi wa Kitengo cha mahala pamoja cha TIC jijini Dar es salaam
leo.
Meneja
Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC), Pendo Gondwe akizungumza
wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kitengo cha mahala pamoja cha TIC jijini
Dar es salaam leo.
Waziri
wa Viwanda na Biashara na uwekezaji, Charles Mwijage akiwa katika picha
ya Pamoja na wadau wa uwekezaji na watendaji kutoka TIC, leo jijini Dar
es Salaam.








Post a Comment