Lengo
la kongamano hilo, litakalofanyika kwa siku mbili jijini Arusha, yaliko
makao makuu ya Mahakama,hiyo ni pamoja na kutathmini kazi za Mahakama
hiyo katika kipindi cha miaka
10 iliyopita.
Kwa
mujibu wa Rais wa Mahaka ya Afrika, Jaji Sylvain Ore,kongamano hilo
litahudhuriwa na wajumbe 150 ambapo mwishoni mwa kongamano watatoa
mapendekezo yatakayo kuza utendaji wa shughuli
za mahakama katika siku zijazo.
Wajumbe wa
kongamano hilo ni pamoja na wasomi ,taasisi za mashirika yasiyo ya
kiserikali,tasisi za Umoja na Afrika (AU) na wawakilishi wa masuala ya
sheria na wale wa taasisi za
haki za binadamu kutoka ukanda wa Afrika .
Aidha
kongamano hilo litafuatiwa na kikao cha ngazi ya juu cha Umoja wa
Afrika kuhusu haki za Binadamu kitakacho fanyika November 23-26, pia
jijini Arusha.
Kikao
hicho, ambacho kinatarajiwa kufunguliwa na Makamu wa Rais Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan, kitapitisha mpango kazi wa miaka 10 kuhusu ukuzaji
na ulinzi wa haki za Binadamu
barani Afrika.
Mahakama
ya Afrika ilianzishiwa mujibu wa kifungu namba Moja cha itifaki ya
mkataba wa mahakama hiyo kwa lengo la kukamilisha na kuimarisha jukumu
la kulinda haki za Tume ya Afrika
ya Haki za Binadamuna Watu barani Afrika.
Hadi
Octoba mwaka huu ni nchi 7 tu kati ya nchi 30 zilizoridhia itifaki ,
ndio zimetoa tamko rasmi la kutambua na kukubali mamlaka ya mahakama
hiyo kuweza kupokea kesi za watu binafsi
na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs).
Nchi hizo 7 ni pamoja na Benin,Burkina Faso ,Cote d’lvoire,Ghana,Mali,Malawi naTanzania.
Aidha
hadi Octoba mwaka huu, jumla ya maombi 119 ya mashauri yali pokelewa na
mahakama hiyo na kesi 32 zimekamilishwa huku kesi 87 zikisubiri
usikilizwaji.

Post a Comment