BY RABI HUME.
KKAMPUNI
ya Paraa Mwanga ambayo inajihusisha na uuzaji wa sola imefanya uzinduzi
wa kampeni ambayo imepewa jina la Tunaangaza Afrika ambayo itawawezesha
watanzania kushiriki na kushinda kwa kutumia 500 tu.
Akizungumza
kuhusu kampeni hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Paara Mwanga, Neela
Krishnamurthy alisema malengo ya kampuni yao ni kusaidia maeneo ambayo
bado hayajafikiwa na huduma ya umeme na hivyo kupitia kampeni hiyo
wananchi watakuwa wakishiriki na kushinda zawadi ya sola za kampuni hiyo
ambazo zitawasaidia kupata mwanga katika nyumba zao.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Paara Mwanga, Neela Krishnamurthy akielezea kampeni ambayo
wameanzisha itakayowawezesha watanzania kushinda vifaa vya umeme wa jua
(sola) vinavyouzwa na kampuni hiyo.
“Kutakuwa
na droo na itafanyika kila wiki na kutakuwa na mshindi, atakuwa
akipatiwa tv na tutakuwa tunampatia sola, kila wiki atakuwa anatangazwa
mshindi mmoja hadi shindano limalizike,” alisema Krishnamurthy.
Nae
Meneja wa Kampuni ya Paraa Mwanga, Michael Mbughi amezungumza kuhusu
kampuni hiyo na kusema kuwa ni kampuni mpya Afrika ambayo kwa kuanza
imeanzia Tanzania ili kuwezesha jamii ya watanzania na zaidi maeneo ya
vijijini kupata vifaa vya umeme ambavyo vinauzwa na kampuni hiyo.
Kampuni ya Paraa Mwanga yafanya uzinduzi wa kampeni Tunaangaza Afrika.
Meneja
wa Kampuni ya Paraa Mwanga, Michael Mbughi akizungumza kuhusu kampuni
hiyo na bidhaa inazoziuza katika maeneo ambayo wanafanya kazi.
“Tuna
mradi ulio na lengo la kuiangaza Afrika na hasa maeneo ya vijijini
ambapo umeme haujafika, tumeona tuanzie Tanzania na baadae tutaenda
katika nchi nyingine, na katika hilo tayari tumeenda Mbagala na kugawa
bure sola katika kaya 10,
“Tutatuma
watu wetu na baadae tutakuwa na mawakala katika mikoa ambayo tutakuwa
tunafanya kazi, bidhaa hizi zipo za aina tofautitofauti na kwa kuanza
tutakuwa katika mikoa na Kagera, Katavi, Sumbawanga na Rukwa,” alisema
Mbughi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Paara Mwanga, Neela Krishnamurthy akimkabidhi msaada wa
redio inayotumia sola mmoja wa wakazi wa kata ya Msongola, wilaya ya
Ilala, Dar baada Paraa Mwanga kufika eneo hilo kwa ajili ya kutoa msaada
huo ikiwa ni sehemu ya kujitambulisha kwa jamii ya watanzania.

Post a Comment