Mwenyekiti
wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss), Anna
Matinde akizungumza katika hafla ya kutimiza Miaka miwili ya
TASWE-Saccos jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Alisema
kuwa TASWE ipo mikoa Tofautitofauti hapa nchini Lengo kuu la hafla ya
Dinner Part Gala ni kuwafikia wanawake wengi zaidi ili kutatua
changamaoto zinazowakabiri hasa kwa upande wa kipato cha mwanamke.
Alisema
kuwa TASWE inamatawi 14, katika matawi hayo wameona watoe elimu ya
Ujasiliamali kwa wanawake wengi zaidi hapa nchini ili kupunguza ongezeko
la utegemezi na waweze kuwa wanawake wajasili na wenye nguvu.
Mshereheshaji,
Angela Bondo akizungumza katika sherehe ya kutimiza miaka miwili ya
TASWE jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Rais
wa Chama cha wenye viwanda Biashara na Kilimo nchini (TCCIA), John
Mayanja akizungumza wakati wa kuadhimisha miaka miwili ya Tanzania
Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss) jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki na kuwataka wanawake watumie fursa zinazojitokeza hasa
kwa wale wanaotaka kusindika juisi za matunda hapa nchini kwa kuwa kuna
matunda mbalimbali inapofikia msimu wake huharibika na kutupwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker, akizungumza na wanawake wakati wa kusheherekea Miaka miwili ya Tanzania
Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss) tangu kuazishwa kwake
na kuwa na wanachama wanawake wengi katika mikoa tofauti tofauti zaidi
ya 10 hapa nchini. Alisema kuwa Wanawake milango imefunguka kwa benki
hiyo hasa wakijiunga kwa makundi ili kupata mikopo yenye riba ya chini
katika benki ya NMB hapa nchini.
Mtoa Maada wakati wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss) ikisherekea Miaka miwili jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wanawake wakiserebuka wakati wa kusherekea miaka miwili ya Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wanawake waliohudhulia katika Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss)Dinner Party Gala na kusheherekea pamoja kutimiza Miaka miwili ya Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss) jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss), Anna Matinde na Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker wakimsikiliza mtoa maada
wakati wa Dinner Paty Gala na kusheherekea miaka miaka miwili ya Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE) jijini Dar es Salaam.
Washiriki wakiwa katika hafla ya Dinner Paty Gala pamoja na Kusheherekea Miaka miwili ya Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss),jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Chama cha wenye viwanda Biashara na Kilimo nchini (TCCIA), John
Mayanja atembelea baadhi ya kazi za wanawake wajasiliamali katika hafla
ya Dinner Paty Gala iliyoambatana na Kusheherekea miaka miwili ya Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss) jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment