Pages

September 15, 2016

SERIKALI KUFUTA UJINGA IFIKAPO MWAKA 2030


 Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda (katikati), akisoma hutuba kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kusoma Vitabu chini ya Hema Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Room to Read, Peter Mwakabwale, iliyoratibu maadhimisho hayo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Haki Elimu, John Kalaghe.


 Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda (kulia), akizungumza kwenye maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Meneja wa Mradi wa Usomaji Room to Read, Mkurugenzi wa Mradi, Room to Read, Juvenalius Kurulatera na Mkurugenzi Mkuu, Haki Elimu, John Kalaghe.
 wadau mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Wanafunzi wakishiriki maadhimisho hayo.
 Maadhimisho yakiendelea.
 Wadau wakifuatilia mada kwenye maadhimisho hayo.
 Mkutano ukiendelea.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mbaruku kutoka wilayani Bagamoyo wakiigiza Igizo la Almas na Jitu kwenye maadhimisho hayo.
 Wanafunzi wakiwa makini kusikiliza mada.
 Wanafunzi kutoka kituo cha kujisomea cha Early Lead Club wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Wadau na raia wakigeni wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Ofisa wa Room to Read kutoka Mikocheni, Veronica Mahenge (kulia), akitoa zawadi ya vitabu kwa wanafunzi waliosoma vizuri vitabu mbalimbali kwenye maadhimisho hayo.

Na Dotto Mwaibale

OFISA Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda kwa niaba ya Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) George Simbachawe, amesema serikali itashirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu kuhakikisha kuwa hadi ifikapo mwaka 2030 wawe wamefuta ujinga nchini.

Mapunda ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya usomaji vitabu kwenye hema yanayoadhimishwa duniani kote. 

Alisema moja ya shabaha iliyopo kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kuhakikisha kila mtoto nchini anapata elimu bure kuanzia darasa la kwaza hadi kidato cha nne.

"Nafahamu shirika lenu la Room to Read limekuwa likitumia mbinu mbalimbali katika kuendeleza elimu bora kwa kuweza kujenga maabara katika shule zetu, kutoa vitabu na mambo mbalimballi katika kupambana na elimu," alisema.

Alisema takwimu za kitaifa za sensa ya makazi na watu katika mwaka 2012 zinaoonesha kuwa asilimia  22 ya watanzania hawezi kusoma na kuandika kwa ufasa, 81.7 ni wenye ya msingi 14.4 ndio wenye elimu ya sekondari na asiimia 2.3 elimu ya  chuo. 

Alisema kiwango hicho kidogo kinasababisha watoto kutokuwa na msingi imara katika kipindi cha mwazoanapoanza shule.

"Kwa mfumo unaofanywa na Room to Read katika kuhakisha wanafunzi wanajua kusomma na kuandika afikapo darasa la tatu ni wazi kuwa serikali tunapaswa kujifunza ili kuhakisha hadi ifikapo 2030 tunakuwa tumefanikiwa kufuta ujinga," alisema Mapunda.

Alisema kaulimbiu ya mwaka huu ya maadhimisho hayo inayosema 'Kuandika yaliyoita, Kusoma yajayo' itumike kutafakari kufuta ujinga.

Awali Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Room to Read, Peter Mwakabwale alisema siku ya usomaji duniani ni siku muhimu kwa wadau wa elimu wakiwemo wanafunzi wenyewe, wazazi, walimu, mashirika yasio ya kiserikali na serikali.

Alisema siku hiyo huadhimishwa kila mwaka  ifakapo Sepemba 9, ikiwa ni kutimiza azimio la Tehrani lilipitishwa mwaka 1965 ambapo kwa mwaka huu wanaadhimisha miaka 50 tangu kuazshwa kwake mwaka 1966.

"Kutokana na kuwepo kwa mitiani ya Taifa ya darasa la saba, sisi Room to Read  na washiriki wezetu tuliona ni vyema kuadhimisha siku hio leo ili kupisha tukio muhimu la wadau wetu," alisema.

Mwakabwale alisema takwimu za Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) za mwaka 2015 zinaonesha hali ya usomaji duniani katika nchi saba Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), Tanzania ni ya pili kwa kuwa na kiwango kikubwa cha watazania wanaojua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa ufasaha kwa asilimia 80.3.

Alisema Nchi ya Burundi inaongoza katika nchi za ukanda huo kwa asilimia 85.6 ya wananchi wake wanajua  kusoma na kuandika kwa kiwango cha juu ukilinganisha na nchi nyingine.

Maadhimisho hayo yalinogeshwa na Taasisi ya Room to Read kwa kufanya maonesho ya vitabu na wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali kupata fursa ya kusoma vitabu na kuulizwa maswali pamoja na kupata zawadi za vitabu
.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...