RAIS
Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, akipokea mfano wa
hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 10 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa
Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (kushoto), ambayo waliiahidi kwa
Msajili wa Hazina kwa ajili ya kuchangia wahanga wa maafa ya tetemeko
la ardhi lililotokea mkoani Kagera. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa PPF,
Lulu Mengele.
RAIS
Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaji Ali Hassani Mwinyi (wa tatu kushoto)
akiongoza matembezi ya kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi
lililotokea mkoani Kagera na maeneo ya jirani. Wengine alioambatana nao
ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Balozi Augustine Maige, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John
Kijazi, Naibu Waziri (Ofisi ya Waziri Mkuu), Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Walemavu, Dkt. Abdallah Possi, Mbunge wa Jimbo la Muleba, Prof.
Anna Tibaijuka pamoja na wengine wengi.
WAFANYAKAZI wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakishiriki matembezi ya hisani ya kuwachangia wahanga wa tetemeko la ardhi.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi
Mkuu wa PPF, William Erio, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
Wafanyakazi wa Mfuko huo, kabla ya kuanza kwa matembezi ya hisani ya
kuwachangia wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akizungumza na
Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia, Mhe Balozi Mbelwa Kairuki
katika viwanja vya Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay wakati wa
shughuli ya kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani
Kagera na maeneo ya jirani.
Wananchi
na Wadau mbalimbali wakifuatilia taarifa ya Maafa na shughuli ya
kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera na
maeneo ya jirani.
No comments:
Post a Comment