Na Faustine Ruta, Bukoba
Bao zote za Kilimanjaro Queens zilifungwa kipindi cha kwanza, Bao la kwanza limefungwa na Asha Rashid dakika ya 22, Bao la pili lilifungwa na Mwanahamisi Omary dakika ya 30 huku
Bao
la tatu lilikuwa la kujifunga wao wenyewe baada ya Mabeki wa Burundi
kujichanganya na Mchezaji Niyonkulu Saidauze kwenye harakati za kutaka
kuokoa mpira kwenye eneo hatari dakika ya 33. Hadi dakika 90
zinamalizika Kilimanjaro Queens ndio walikuwa wababe kwa kutoka na
ushindi wa bao 3-0. Mchezo huo wa kirafiki wa Kimataifa uliokuwa ni moja
ya Timu zote mbili kujiandaa na Michezo ya CECAFA Nchini Uganda. Na
Kesho Timu zote mbili zinaelekea jijini Jinja, Nchini Uganda.
Michuano
ya CECAFA ya kuwania Kombe la Afrika Mashariki na Kati itafanyika kwa
siku tisa kuanzia Septemba 11, 2016 jijini Jinja, Uganda.
Kwa mujibu wa CECAFA, Tanzania ambayo inaongoza kwa ubora wa viwango vya
Mpira wa Miguu kwa nchi za Afrika Mashariki imepangwa kundi B ikiwa
pamoja na timu za Rwanda na Ethiopia wakati kundi A litakuwa na timu za
Kenya, Burundi, Zanzibar pamoja na mwenyeji Uganda.
Tanzania itafungua michezo hiyo kwa kucheza na Rwanda Septemba 12, 2016
kabla ya kucheza na Ethiopia Septemba 16, 2016. Rwanda na Ethiopia
zitacheza Septemba 14, 2016 wakati kundi A Zanzibar itakata utepe kwa
kucheza na Burundi na siku hiyohiyo, Uganda itacheza na Kenya.
Michezo mingine ya kundi A itakuwa ni kati ya Burundi na Kenya
zitakazocheza Septemba 13, 2016 ambako siku hiyohiyo Zanzibar itacheza
na Uganda. Septemba 15, Kenya itacheza na Zanzibar na Uganda itafunga
hatua ya makundi kwa siku hiyo kwa kucheza na Burundi.
Nusu fainali itafanyika Septemba 18, kabla ya fainali kufanyika Septemba
20, 2016 ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu na nne.
Mashindano ya CECAFA kwa timu za wanawake yanafanyika kwa mara ya kwanza
jambo linaloleta tafsiri kuwa michuano hiyo inaweza kuinua soka la
wanawake kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Tanzania inatarajiwa
kuanza kambi Septemba mwanzoni kwa mazoezi ya kwenda na kurudi nyumbani
kwa wiki moja na baadaye wataingia kambini moja kwa moja tayari kwa
safari ya Uganda.
Mashabiki jukwaa kuu
Waamuzi wa mtanange katikati ni Ahmada Simba ambaye ndiye alikuwa Mwamuzi wa kati
Kipa wa Burundi
Mwisho wa mchezo walipata picha ya pamoja kwani Michezo ni Furaha
No comments:
Post a Comment