Kiongozi
wa ujumbe toka Sweden, Bi. Matilda Irnkarns (kushoto) akikabidhi zawadi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo.
|
Nteghenjwa Hosseah –Arusha
MKOA
wa Arusha umeanza kujipanga katika utaratibu wa kulinda mji kwa kutumia
teknolojia ya kisasa ya CCTV – Camera ili kuimarisha usalama wa mji “Safe
City”, Mfumo huu utawezeshya Mji kulindwa masaa 24 dhidi ya uhalifu kwa raia,
wawekezaji na watalii.
Kauli
hiyo ilitolewa leo mjini hapa na Mkuu wa Mkoa huo Mrisho Gambo ofisini kwake
mara baada ya kutembelewa na Balozi wa Sweden nchini, Bi. Katarina Rangnite
aliyeambatana na Ujumbe wake wa Wabunge kutoka Nchini Sweden.
Akizungumza
na ujumbe huo RC Gambo alisema, mkoa huo tayari umekwisha kuonyesha nia ya
kuwekeza katika mfumo huo ili kuwaongezea wananchi na mali zao usalama zaidi.
“Nia
yetu ni kuona hali ya usalama katika mkoa wa Arusha ikiwa ya juu sana ili kuendelea kuwavutia watalii zaidi kutoka
nchi mbalimbali Duniani. Malengo yetu ni kuwa na mifumo itakayoulinda mkoa wetu
kwa Saa 24 na mwaka mzima,” alisema RC
Gambo na kuongeza:
“Hatua
hii itaongeza ulinzi kwa raia na mali zao, pia kwa wawekezaji waliopo
mkoani kwetu na watalii wanaokuja kutembelea hifadhi na vivutio mbalimbali
kwani Arusha ndio kitovu cha utalii hapa nchini,” alisema.
Kwa
upande wake Balozi Rangnite ambaye kiongozi
wa msafara huo uliojumuisha pia wabunge kutoka Bunge la Sweden wanaowakilisha
Kamati ya Kilimo na Mazingira, alikubaliana na nia ya kuwekeza kwenye mfumo wa
usalama wa mkoa wa Arusha.
Balozi
Rangnite alimueleza Mkuu wa Mkoa Gambo kwamba, nchi ya Sweden inayo wataalamu
waliobobea katika mifumo hiyo ya usalama wa miji hivyo alimuomba Gambo
kuwasilisha kwake maandiko ya vitu vinavyohitajika ili kuwezesha mradi huo
kutekelezwa.
“Tukipata
maandiko mbalimbali ya mradi tunaweza kuangalia ni wapi Serikali ya Sweden
inaweza kuwekeza ikiwamo kusaidia kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili,”
alisema Balozi Rangnite.
Aidha
Gambo alitoa ombi kwa Balozi wa Sweden
kushirikiana na Mkoa wa Arusha kwenye kampeni ya kulinda vyanzo vya Maji ili
kuwezesha mradi mkubwa wa maji unaosimamiwa na mamlaka ya maji safi na maji taka
(AUWSA) kutekelezwa kwa mafaniko makubwa. Itakumbukwa kwamba imepatiwa Bil 476
ili kumaliza tatizo la maji Jiji hapa.
Katika
ziara ya ujumbe huo pamoja na mambo mengine ulikuwa na lengo la kuangalia fursa mbalimbali
za uwekezaji katika Kilimo, Mazingira na maeneo muhimu kutoka mkoani Arusha.
Ujumbe
huo kutoka Sweden ukiongozwa na Balozi Rangnite uliridhishwa na kuvutiwa na
maeneo ya utalii yaliyopo katika mkoa huo yakiwamo pia mazingira rafiki
yanayoruhusu uwekezaji kwa jamii yao.
No comments:
Post a Comment