Viongozi
Wakuu pamoja na Sekretieti ya Mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja
baada ya ufunguzi wake, katikati mwenye suti ni Waziri Mkuu wa
Mauritius Sir Anerood Jugnauth.
Ujumbe
wa Tanzania walioshiki Mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na
Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid
katikati kulia Mwenyekiti wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Mussa Zungu na kushoto Dk Raphael Chegeni.Kutoka kushoto Maryam
Rajab, Mbarikiwa Masinga, Mhe,Maria (MB) Mhe. Raphael Chegeni (MB)Mhe
Juma Hamad Omar (MB) Mhe Simai Mohammed Said (BLW) Aziza Makwai.
Spika
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akibadilishana
mawazo na Wajumbe kutoka Tanzania kabla ya kuaza kwa Mkutano huo.
Mjumbe
wa Mkutano wa Nchi za Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Mhe. Simai
Mohammed Said, akiwasilisha Mada wakati wa Mkutano huo inayozungumzia
Suala la Nishati kwa Bara la Afrika, uliofanyika nchini Mauritius
Balaclava.
Spika
wa Baraza la Wawkilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akiwa na
Wajumbe kutoka Tanzania wakishirika katika Mkutano huo wakifuatilia Mada
zinazowasilishwa na Wajumbe wakati wa Mkutano huo nchini Mauritius.
Mtoto
wa Mfalme wa Lesotho HRH Prince Seeiso B Seeiso, Raisi wa Senate na
Mwenyekiti wa Kamati ya Biashara kutoka Bunge la Falme ya nchi ya
Lesotho akichangia mada iliyowasilishwa na Tanzania inayohusiana na
nishati ya umeme.
Mjumbe
wa Sekterieti kutoka Tanzania Aziza Mwakwai kushoto akimsaidia Spika wa
Rwanda wakati wa Kikao hicho za kuwasilisha Mada kwa Nchi husika.
Spika
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid na Mwakilishi
wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said wakipitia makabrasha
yao kabla ya kuaza Kikao cha Kanda ya Afrika Mashariki. katika ukumbi
wa Hoteli ya Meridian Mauritius
Mjumbe
wa Mkutano wa Nchi za Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Mhe. Simai
Mohammed Said akizungumza na Spika wa Bunge la Mauritius na Rais wa
Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Hon Mrs.Santi Bai
Hanoomanjee. kulia kwake Katibu wa Bunge la Mauritius.
Spika
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid kutoka kulia
akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Kenya Mhe.Justin Muturi, Spika
wa Uganda Mhe Rebecca Kadaga na Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Zungu akimwakilisha Spika wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe Job Ndungai.
Spika
la Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid (katikati)
akifurahia jambo wakati wakibadilishana mawazo na Wajumbe wa Mkutano
huo, kushoto Spika wa Bunge la Uganda Mhe. Rebecca Kadaga na Mhe Simai
Mohammed Said Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar, wakiwa nje ya
Ukumbi wa Mkutano baada ya kuahirishwa kwa mapumziko ya mchana.
Katibu
wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano la Tanzania ambaye pia Katibu wa Nchi
za Jumuiya ya Madola Dk Thomas Kashillilah wa tatu kutoka kulia mwenye
suti, akizungumza na Wajumbe wa Sekterieti ya Jumuiya ya Kanda ya Afrika
wakiwa nje ya Ukumbi wa Mkutano huo uliofanyika Nchini Mauritius.
Mwakilishi
kutoka Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akiwa katika picha ya pamoja
na Wajumbe wa Mkutano huo, pamoja na Spika wa Bunge la Kenya Mhe Justin
Muturi mwenye kaunda suti pamoja wa Wawakilishi kutoka Kisiwa cha
Rodrigues Mauritius.
Spika
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akiwa na Mhe
Simai Mohammed Said wakiwa katika eneo maarufu la Kitalii nchini
lijulikanali kwa jina la Trou Aux Cerfs (Valcano in Vacoas - Phoenix,
Mauritius).
Spika
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zuberi Ali Maulid akiwa na
Wajumbe wa Mkutano huo wakitembelea Kiwanda cha kufulia Umeme na Sukari nchini Mauritius wakipata maelezo kutoka kwa Kiongozi wa Kiwanda hicho
cha Omnicane Limited.
Msanii
wa Sanaa za kutengeneza Boti kwa ajili ya Watalii wanaotembelea Nchi
hiyo akiwa katika harakati za kutengeza boti zinazopatika katika eneo
la Curepipe Mauritius hutengenezwa kwa mbao kama majahazi ya Zanzibar.
Sanamu
la pili refu duniani baada la Nchini India lijukanalo kwa jina Lord
Shiva Nchini Mauritius likiwa katika maeneo ya Ganga Talao.
Mandhari ya kutoka juu ya bustani ya Trou Aux Cerfs.
Imetayarishwa na Zanzinews.com
Imetayarishwa na Zanzinews.com
No comments:
Post a Comment