Pages

August 30, 2016

Waziri Nape azindua michezo ya Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika


 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa tatu kulia) akiingia katika Uwanja wa Michezo wa Taifa tayari kwa ufunguzi wa mashindano ya michezo inayoshirikisha Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO), kushoto kwake ni Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba na kulia kwake ni Rais wa Chama cha Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda na Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Richard Gundane.

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) akiimba wimbo wa Taifa wakati wa ufunguzi wa   mashindano ya michezo inayoshirikisha Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO), wa pili kushoto ni Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba, na kushoto ni Katibu kutoka Ofisi ya Uhamiaji wa Ubalozi wa Malawi Bw. Michael Gama.  Wa pili kulia ni Rais wa Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda na kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Richard Gundane.
 Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba akisoma risala wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO), kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye.

 Rais wa Chama cha  Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Umoja wa Vyama vya walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye, na kushoto ni Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)Bw. Gratian Mukoba.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa salamu kwa wanamichezo ambao ni walimu wanaowakilisha nchi za kusini mwa Afrika wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo leo jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Rais wa  Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda na kushoto ni Rais wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba.
 Kikosi cha Brass Bendi ya Polisi Nchini wakiongoza maandamano ya wanamichezo ambao ni walimu kutoka nchi za Kusini mwa Afrika kuingia uwanjani wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo leo Jijini Dar es Salaam.
 Wanamichezo ambao ni walimu kutoka Zambia wakiingia uwanjani wakati wa ufunguzi wa mashindano yaliyoshirikisha nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) leoJijiniDar es Salaam.
 Wanamichezo ambao ni walimu kutoka Afrika ya Kusini wakiingia uwanjani wakati wa ufunguzi wa mashindano yaliyoshirikisha nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) leo Jijini Dar es Salaam.
 Wanamichezo ambao ni walimu kutoka Tanzania wakiingia uwanjani wakati wa ufunguzi wa mashindano yaliyoshirikisha nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) leoJijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akifyatua baruti juu kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano ya Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika(SATO) leo JijiniDar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na wachezaji wakati wa  ufunguzi  wa mashindano ya  Vyama Vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) leo Jijini Dar es Salaam.Picha Na:Lorietha Laurence WHUSM.


Lorietha Laurence - WHUSM

Michezo ni mojawapo ya nyenzo muhimu katika kuimarisha ushirikiano  na mahusiano baina ya nchi na nchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati wa ufunguzi wa michezo ya Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) ambayo imeanza rasmi leo Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Nnauye amesema kuwa ni fahari kubwa kwa serikali ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa kuwa inatoa fursa kwa wageni na wenyeji kujumuika kwa pamoja na kujifunza mbinu mbalimbali za kimichezo.

“Kuunganisha nchi na nchi si kazi rahisi lakini kupitia michezo imekuwa ni jambo rahisi kwa kuwa inawafanya kuwa na umoja uliothabiti na hivyo kuimarisha mahusiano baina ya nchi husika” alisema Mhe. Nnauye

Aidha Mhe. Nnauye aliwataka washiriki wasiishie kwenye michezo tu bali pia watumie  fursa ya kuwepo nchini kwa kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo katika Jijini la Dar es Salaam ikiwemo Makumbusho ya Taifa pamoja na Bagamoyo ambako kuna historia kubwa ya nchi.

Naye Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba ameeleza kuwa mashindano hayo ni muhimu kwa walimu kwa kuwa yanawasiadia kuimarisha afya pamoja na kushirikiana katika kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili  sekta hiyo.

“kupitia michezo hii tunaimarisha afya pamoja na kujadili changamoto  mbalimbali wanazokumbana nazo walimu ikiwemo ukosefu wa walimu wa masomo ya hesabu na sayansi na namna ya kutatua tatizo hilo “ alisema Bw. Mukoba.

Kwa upande wake Rais wa Vyama vya Walimu  wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda amesema kuwa kupitia michezo hiyo walimu hujifunza tamaduni mbalimbali baina yao ukizingatia elimu ndio msingi wa maendeleo.

Mashindano haya ya Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) yanafanyika kwa mara ya sita huku Tanzania ikiwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa mara ya kwanza ikihusisha nchi za Namibia, Lesotho, Botswana, Zimbabwe, Zambia, Malawi, Afrika ya Kusini, Swizland na Tanzania

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...