Wekundu
wa Msimbazi Simba wamelazimishwa sare goli 1-1 kwenye mchezo wa
kimataifa wa kirafiki dhidi ya URA ya Uganda uliochezwa kwenye uwanja wa
taifa.
URA
walianza kupata bao lililofungwa na Nkugwa Elkanah 19kipindi cha kwanza
lakini Jonas Mkude alisawazisha bao hilo dakika ya 31 kwa kuunganisha
mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na beki wa kushoto Mohamed Hussein
‘Zimbwe Jr.
Mechi
hiyo ya kirafiki ya kimataifa ni ya pili kwa Simba baada ya klabu hiyo
kucheza mchezo mwingine August 8 dhidi ya AFC Leopards ya Kenya wakati
wa maadhimisho ya Simba Day.
Katika
mcchezo dhidi ya Leopards ya Kenya, Simba ilipata ushindi wa magoli 4-0
yaliyofungwa na Ibrahim Ajib ambaye alifunga mawili, Shiza Kichuya na
Laudit Mavugo lakini nyota hao hawakufanikiwa kufunga bao.
Simba
inajiandaa na ligi kuu ya soka Tanzania bara inayotarajiwa kuanza Agust
20, Simba itaanzia kwenye uwanja wa taifa dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara.







Post a Comment