Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas
Mushi (kushoto) akimkabidhi tuzo kwa niamba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa
shirika hilo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
(kulia) iliyotolewa na TTCL kwa mwanariadha, Alphonce Simbu aliyefanya
vizuri katika mashindano ya Olimpiki 2016 yaliofanyika jijini Rio De
Jeneiro nchini Brazil hivi karibuni. Wengine wanaoshuhudia ni baadhi ya
viongozi wa vyama vya riadha Tanzania.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas
Mushi (kulia) akimkabidhi tuzo mwanariadha, Alphonce Simbu aliyefanya
vizuri katika mashindano ya Olimpiki 2016 yaliofanyika jijini Rio De
Jeneiro nchini Brazil kwa niamba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.
Wanaoshuhudia katikati ni baadhi ya wanariadha waliyoiwakilisha Tanzania
katika mashindano hayo.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas
Mushi (wa kwanza kulia kulia) akimkabidhi tuzo mwanariadha, Alphonce
Simbu aliyefanya vizuri katika mashindano ya Olimpiki 2016 yaliofanyika
jijini Rio De Jeneiro nchini Brazil kwa niamba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa
TTCL. Wanaoshuhudia katikati ni baadhi ya wanariadha waliyoiwakilisha
Tanzania katika mashindano hayo.
Kushoto ni wachezaji wa timu ya Taifa Tanzania walioshiriki katika
mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2016 yaliofanyika hivi karibuni jijini
Rio De Jeneiro nchini Brazil wakirejesha bendera ya taifa kwa Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (wa tatu kulia) kwenye
hafla ya chakula cha jioni kuwapongeza wachezaji iliyofanyika jijini Dar
es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande
(katikati) akizungumza kuwapongeza wachezaji hao. Kushoto ni Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na Meneja Uhusiano wa
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Mushi (kulia) wakiwa katika
hafla hiyo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
akimkabidhi king'amuzi cha DSTV mwanariadha Alphonce Simbu (kushoto)
aliyefanya vizuri katika mashindano ya Olimpiki 2016 yaliofanyika jijini
Rio De Jeneiro nchini Brazil. Kampuni ya TTCL imetoa fedha kwa
washiriki wote wa mchezo huo ikiwa ni ishara ya kuwapongeza na kuwatia
moyo ili waweze kufanya vizuri zaidi katika mashindano yajayo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
akizungumza kwenye hafla ya chakula cha jioni kuwapongeza wachezaji wa
timu ya Taifa Tanzania walioshiriki katika mashindano ya Olimpiki ya
mwaka 2016 yaliofanyika hivi karibuni jijini Rio De Jeneiro nchini
Brazil. Kampuni ya TTCL imetoa fedha kidogo kwa washiriki wote wa mchezo
huo ikiwa ni ishara ya kuwapongeza na kuwatia moyo ili waweze kufanya
vizuri zaidi katika mashindano yajayo.
Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Antony Mtaka akizungumza
katika hafla ya kuwapongeza wanamichezo waliounda timu ta Taifa ya
Tanzania kushiriki mashindano ya Olimpiki 2016 Rio.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas
Mushi (kulia) akizungumza kabla ya kukabidhi tuzo kwa niamba ya Ofisa
Mtendaji Mkuu wa shirika hilo kwa mwanariadha, Alphonce Simbu aliyefanya
vizuri katika mashindano ya Olimpiki 2016 yaliofanyika jijini Rio De
Jeneiro nchini Brazil hivi karibuni. Tuzo ya TTCL pamoja na zawadi kwa
wanariadha walioshiriki mashindfano hayo ilikabidhiwa na Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye. Kulia ni baadhi ya
maofisa wa TTCL wakiwa na tuzo hiyo.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas
Mushi (kushoto) akimkabidhi tuzo kwa niamba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa
shirika hilo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
(kulia) iliyotolewa na TTCL kwa mwanariadha, Alphonce Simbu aliyefanya
vizuri katika mashindano ya Olimpiki 2016 yaliofanyika jijini Rio De
Jeneiro nchini Brazil hivi karibuni. Wengine wanaoshuhudia ni baadhi ya
viongozi wa vyama vya riadha Tanzania.
Baadhi ya maofisa wawakilishi wa TTCL wakipiga picha ya pamoja na
timu ya riadha iliyoiwakilisha Tanzania mashindano ya Olimpiki 2016 Rio,
nchini Brazil.
KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) inafanya mazungumzo na vyama vya
mchezo wa riadhaa nchini pamoja na wachezaji wa mchezo huo ili kuandaa
mpango utakaowawezesha wanaridha kufanya mazoezi ya kutosha na hatimaye
kufanya vizuri katika mashindano yao mbalimbali. Kauli hiyo imetolewa
jana na Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemas Mushi kwa niamba ya Ofisa
Mtendaji Mkuu wa shirika hilo alipokuwa akitoa tuzo kwa mmoja wa
wanariadha, Alphonce Simbu aliyefanya vizuri katika mashindano ya
Olimpiki 2016 yaliofanyika jijini Rio De Jeneiro nchini Brazil hivi
karibuni. Mwanariadha Simbu alishika nafasi ya tano katika mbio za
marathoni na kuvunja rekodi kwa wanariadha wa Tanzania.
Kampuni
ya TTCL mbali ya kutoa tuzo na fedha zitakazomsaidia mchezaji huyo
akiwa mazoezini kwa sasa, imetoa fedha kidogo kwa washiriki wote wa
mchezo huo ikiwa ni ishara ya kuwapongeza na kuwatia moyo kutokata tamaa
ili waweze kufanya vizuri zaidi katika mashindano mengine yajayo.
"...Kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura TTCL
tumejiunga na wadau wengine wa michezo katika kuwapongeza wanamichezo
wa timu ya Taifa ya Tanzania walioshiriki mashindano ya Olimpiki 2016
yaliofanyika jijini Rio De Jeneiro nchini Brazil, TTCL kwa nafasi yetu
tumejiweka mstari wa mbele katika kuwasaidia wanamichezo wa riadha,
tumejitolea kufanikisha timu ya riadha katika kukaa vizuri kimichezo..,"
alisema Mushi.
"...Katika
kipindi hiki cha michezo 2016 tumejitolea kuifanikisha timu ya riadha
kuweza kushiriki vizuri katika programu za mazoezi, leo wakati wanarejea
tumewaunga mkono kwa kutoa tuzo na fedha kwa msindi aliyefanya vizuri
mwaka huu na pia kutoa fedha kwa wanamichezo wetu zitakazo wawezesha
kufanya vizuri katika mazoezi yao, huu ni mwanzo lengo letu ni kwamba
tutaweka utaratibu mzuri wa kuzungumza na vyama pamoja na taasisi
zinazosimamia michezo hii ili kuona tunatengeneza utaratibu mzuri zaidi
ambao ni endelevu utakaosaidia kukua kwa mchezo huu,"
alisisitiza
meneja uhusiano huyo. Tuzo ya TTCL kwa Alphonce Simbu na fedha kwa
wanariadha hao zilikabidhiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Nape Nnauye ambapo aliwapongeza wanamichezo wote wa timu ya
tanzania iliyokwenda nchini Brazil kwenye mashindano ya Olimpiki 2016
kwa uzalendo waliouonesha kwa taifa licha ya changamoto anuai. Waziri
Nnauye aliwaomba Watanzania kutowakejeli wanamichezo hao kwa maneno ya
kuwakatisha tamaa na badala yake kuungana kuwapongeza na pia kutoa
ushauri kwa wadau wa michezo ili Tanzania iweze kufanya vizuri katika
mashindano yajayo, ikiwa ni pamoja na vyama vya michezo kusaidia
kyuongeza idadi ya wachezaji wa timu ya Tanzania.
Kampuni
ya Multichoice Tanzania pia iliungana na TTCL na kuwazawadia ving'amuzi
vya DSTV vilivyolipiwa kwa muda wa miezi sita wanamichezo wote wa timu
ya Tanzania iliyoshiriki katika mashindano ya Olimpiki mwaka 2016,
pamoja na kumsaidia kumuwezesha mwanariadhaa Simbu programu za mazoezi
kwa muda wa mwaka mmoja akiwa kama balozi wa kampuni hiyo. Timu ya Taifa
ya Tanzania iliyoshiriki katika mashindano ya Olimpiki mwaka 2016
ilikuwa na wanamichezo saba, ambapo wanamichezo wanne walishiriki
riadha, wawili waogeleaji na mmoja alishiriki mchezo wa judo.
No comments:
Post a Comment