Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Diamond Jubilee kwa ajili ya
Ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya
Usajili wa Makandarasi nchini CRB.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wakandarasi, Wahandisi na wadau mbalimbali wa sekta ya Ujenzi kabla ya kufungua rasmi Mkutano wa Siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini CRB uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipewa maelezo kuhusu katapila linalotumika katika kazi mbalimbali za ujenzi mara baada ya kufungua mkutano wa siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati akikagua baadhi ya mitambo na magari mbalimbali katika maonesho ya vifaa hivyo vinavyotumika katika sekta ya ujenzi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia vifaa vya ujenzi katika moja ya mabanda mara baada ya kufungua mkutano wa siku mbili wa Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi jijini Dar es Salaam.

Wadau mbalimbali wa Sekta ya Ujenzi wakiwemo Wahandisi na Wakandarasi
wakipiga makofi wakati wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano huo wa
Mashauriano wa CRB jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU.
RAIS Magufuli akemea vitendo vya ruswa kwa wakandarasi
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli
amewataka wakandarasi nchini kujiepusha na vitendo vya rushwa ili
kulisaidia Taifa kupiga hatua ya kimaendeleo.
Mhe.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akifungua Mkutano wa
Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini (CRB) uliofanyika
jijini Dar es Salaam.
“Mnaweka
viwango vikubwa vya fedha kwenye miradi ili muweze kupata fedha ya
kutoa rushwa, kwa nini mnafanya hivyo?”amewauliza Mhe. Rais Magufuli na
kuwambia kuwa kama wapo watumishi wa serikali wanaowaomba rushwa ili
wapate kazi waitaarifu Takukuru mara moja ili wachukuliwe hatua.
Mhe.
Rais amewataka wakandarasi wazawa wajipange kufanya kazi na kuwaonya
wasiwe wanaweka viwango vikubwa ambavyo vinachangia kuwakosesha zabuni.
Akitoa
mfano, Mhe. Magufuli alisema katika ujenzi wa mahakama za mwanzo hapa
nchini, jengo moja lilikadiriwa kukamilika kwa milioni 200 lakini
wakandarasi wa Tanzania walioomba zabuni hiyo walitoa kiwango cha kati
ya shilimgi milioni 670 na bilioni 1.4. Amesema kwa jinsi hii hata mtu
awe na huruma ya namna gani hawezi kuwapa kazi.
Amesema
serikali yake itawajali kwanza wakandarasi wa hapa nchini lakini
akawataka wajipange na pengine waungane ili kufanya kazi kwa pamoja.
Aidha,
Mhe. Rais amesema ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi
Tanzania unakaribia kuanza lakini akauliza wakandarasi wa hapa nchini
wamejipangaje katika kushiriki ujenzi huo.
Kuhusu
ulipaji wa madeni ya wakandarasi, Mhe Rais amesema, serikali yake
imekuwa ikilipa madeni hayo na itaendelea kufanya hivyo hadi deni
litakapoisha. Amesema kwa kuanza serikali imelipa bilioni 650 na baadaye
ikatumia bilioni 462 kutoka Mfuko wa Barabara kuwalipa wakandarasi.
Amesema
wakandarasi ni watu wa muhimu sana katika maendeleo ya Taifa na ni
injini ya maendeleo kwani wako kila sekta ya maendelo. Amesema kwa mfano
wako katika ujenzi wa mioundombinu, kwenye zana za kilimo,kwenye
uvuvi, na pia usafirishaji wakandarasi hawakosekani.
No comments:
Post a Comment