Pages

May 5, 2016

Mtangazaji alihaidi kama Leicester itashinda EPL atafanya TV show yake na nguo ya ndani, ishu imefika kwa waziri mkuu

Bunge la Uingereza May 4 ilikuwa kama kuna vichekesho baada ya mjadala kuzuka ndani ya bunge hilo kutokana na mmoja kati ya wabunge kuuliza swali kwa waziri mkuu wa Uingereza, wakati wa muda wa maswali na majibu kuhusu mtangazaji wa BBC Gary Lineker kutotimiza ahadi yake.
o-GARY-LINEKER-facebook
Gary Lineker
Gary Lineker aliwahi kuhaidi kuwa kama Leicester City itafanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu Uingereza, basi atafanya TV show yake akiwa na nguo ya ndani pekee, kitendo ambacho bado hajakitekeleza, mbunge Keith Vaz ambaye ni shabiki mkubwa wa Leicester aliingia bungeni na Scarf ya Leicester na wakati wa maswali na majibu alimuuliza swali waziri mkuu wa Uingereza David Cameron.
gaaa
Keith Vaz alihoji kuhusu ahadi ya mtangazaji huyo wa BBC Gary Lineker ambaye amewahi kuichezea Leicester City miaka ya nyuma katika nafasi ya ushambuliaji, kuwa alihaidi kufanya Tv show yake akiwa na nguo ya ndani, waziri mkuu wa Uingereza David Cameron alimjibu na kumwambia Lineker anastahili kutekeleza ahadi yake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...