Waziri
wa Fedha wa zamani, Basil Pesambili Mramba (kushoto), akijipangusa jasho
wakati akienda kusaini fomu kwa Ofisa Afya Mazingira wa Hospitali ya
Serikali ya Sinza Palestina, Miriam Mong (kulia), baada ya kufanya
usafi katika maeneo kadhaa ya hospitali hiyo Dar es Salaam leo asubuhi,
ikiwa ni adhabu ya kutumikia kifungo cha nje hadi Novemba 5 mwaka huu.
Mawaziri
wa Fedha wa zamani, Basil Mramba (kushoto) na Daniel Yona wakienda
kusaini fomu kwa Ofisa Afya Mazingira wa Hospitali ya Serikali ya Sinza
Palestina, Miriam Mong baada ya kufanya usafi katika maeneo kadhaa ya
hospitali hiyo Dar es Salaam leo asubuhi, ikiwa ni adhabu ya kutumikia
kifungo cha nje hadi Novemba 5 mwaka huu.
Na Dotto Mwaibale
ALIYEKUWA
Waziri wa Fedha, Basil Mramba na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini
Daniel Yona wanaendelea kutumikia kifungo cha nje kwa kufanya usafi
katika Hospitali ya Sinza Palestina.
Yona na
Mramba wanaendelea na hatua hiyo baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisuu
kuridhia kutumikia kifungo hicho baada ya Magereza kuwasilisha orodha
ya majina ya wafungwa ambapo wao ni miongoni mwa watu ambao walionekana
kuweza kutumikia kifungo hicho cha nje kitakachoisha Novemba 5 mwaka.
Akizungumza
Dar es Salaam leo asubuhi, Ofisa Afya Mazingira wa Hospitali hiyo Miriam
Mong ambaye pia anawasimamia alisema wamekuwa wakionesha ushirikiano
katika kutimiza majuku waliyopatiwa.
"Wanaanza
saa mbili asubuhi hadi saa nne, lakini wamekuwa wakionesha ushirikiano
kila wanapofika katika kutimiza majukumu yao," alisema.
Alisema leo
walifanya usafi katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya kupigadeki katika
makorido ya wodi ya wazazi na maeneo ya nje na kesho watafanya katika
wodi ambayo wanatibiwa wagonjwa wa kuja na kuondoka OPD na wanafanya
usafi kwa awamu," alisema.
Alisema endapo ikitokea wakafanya usafi katika eneo fulani ambalo halikung'aa watalazimika kurudia.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment