Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akimkaribisha Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin Wiliam Mkapa Ikulu
jijini Dar es Salaam. 
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin William Mkapa
Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akimkaribisha Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini
Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07
Januari, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu
ya tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji
Joseph Sinde Warioba Ikulu Jijini Dar es salaam.
Akizungumza
mara baada ya Mazungumzo hayo Rais Mstaafu Mkapa amesema lengo la
kukutana na Rais Magufuli ni kumpongeza kwa dhamana aliyopewa na
watanzania kuiongoza nchi, kuunda serikali na kumtakia heri ya Mwaka
Mpya.Rais Mstaafu Mkapa pia amemhakikishia Rais Magufuli kuwa yupo
tayari kutoa ushirikiano wakati wote ama kufanya kazi yoyote endapo
atahitajika kufanya hivyo.
Kwa
upande wake Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba pamoja na
kumtakia heri ya Mwaka Mpya, amempongeza Rais Magufuli kwa jinsi
alivyoanza kazi vizuri hususani katika kusimamia ukusanyaji wa mapato,
kubana matumizi na kuelekeza matumizi kwenye maeneo muhimu ambayo
yanawahusu wananchi yakiwemo afya na maji.Jaji Warioba ameongeza kuwa
Watanzania wote wanapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi kubwa
anazofanya, ambazo ni kukomesha rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya
madaraka na wizi wa mali ya umma.
"Lazima
kila mmoja amuunge mkono Rais, tusije tukamuachie, pale ulipo kama ni
mambo ya rushwa uanzie hapo hapo, kama ni mambo ya matumizi mabaya ya
madaraka anzia hapohapo, tusije tukamuachia Rais pekee yake, yeye awe
kiongozi wetu, lakini watanzania wote tushughulike na matatizo hayo"
alisisitiza Jaji Warioba.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
07 Januari, 2016


Post a Comment