






New Orleans, Marekani
WATU wapatao
16 wakiwa kwenye mkusanyiko wamejeruhiwa baada ya kufyatuliwa risasi na
watu wasiojulikana mjini New Orleans nchini Marekani.
Tukio hilo
limetokea jana jioni amapo watu wapatao 500 walikuwa wamekusanyika
kwenye makundi mawili katika bustani ya Bunny Friend Park mjini New
Orleans. Kundi la kwanza walikwenda kutazama video iliyokuwa ikiandaliwa
bustanini hapo, na kundi la pili wakienda kwenye gwaride la wakazi wa
mtaa huo ndipo kikundi kingine cha watu watano wasiofahamika wenye
silaha akiwemo mwanamke mmoja walizuka na kuanza kuwashambulia umati huo
kwa kuwarushia risasi kisha kujeruhi 16.
Baada ya
taharuki hiyo polisi wa eneo hilo walifika na kuanza kujibizana nao
risasi ndipo wakaamua kukimbia, polisi waliwachukua majeruhi hao na
kuwapeleka hospitali.
Shuhuda
mmoja wa tukio hilo amekaririwa akisema kuwa, mmoja kati ya wavamizi hao
alijipenyeza katikati ya umati huo na kufyatua risasi mara 10, baadaye
waliingia watu wanne wakiwa na silaha pia, nao wakaanza kushambulia
umati huo.
No comments:
Post a Comment