Miongoni
mwa nyumba zilizopo Mtaa wa Kilimahewa Manispaa ya Ilemela Mkoani
Mwanza ambazo huathirika na kero ya Maji kuingia ndani pindi mvua
zinapoanza kunyesha.
Pichani
ni mmoja wa wakazi wa Kilimahewa akitoa maji ndani ya nyumba yake
kutokana na mvua iliyoanza kunyesha majira ya saa kumi na mbili alfajiri
hii leo. Hadi tunaenda hewani (saa 10:30 asubuhi) Mvua hiyo inaendelea
kumiminika mdogomdogo.
Picha na Loyce Nhaluke
Mbali
na Kilimahewa, Pia wakazi wa Mabatini Jijini Mwanza hukumbwa na kero ya
Mafuriko wakati wa Mafuriko na kwa miaka mingi juhudi za kuwahamisha
zimekuwa zikigonga mwamba linapokuja suala la kuwatafutia makazi mapya.
Mara kadhaa mafuriko katika maeneo hayo yamekuwa yakisababisha athari mbalimbali ikiwemo vifo.
Maji hadi ndani, hakika ni hatari
Maji yakitolewa ndani
Kilimahewa Manispaa ya Ilemela
Binagi Media Group, Kwa Pamoja Tuijuze Jamii
No comments:
Post a Comment