Pages

November 16, 2015

WAFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB WAKISHIRIKI MICHEZO MBALIMBALI KATIKA SIKU YA FAMILIA DAY

Wafanyakazi wa  Benki ya CRDB  mkoa wa Arusha wakifanya mazoezi ya viungo katika viwanja vya Olasiti Garden leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za wateja.

Wafanyakazi wa  Benki ya CRDB mkoa wa Arusha  wakishindana kuvuta kamba katika viwanja vya Olasiti Garden leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za wateja

Wafanyakazi wa  Benki ya CRDB mkoa wa Arusha  wakishindana kuvuta kamba katika viwanja vya Olasiti Garden leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za wateja

Watoto wakifurahia michezo mbalimbali   katika viwanja vya Olasiti Garden leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za wateja.

Watoto wakifurahia michezo mbalimbali   katika viwanja vya Olasiti Garden leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za wateja

Watoto wakifurahia michezo mbalimbali   katika viwanja vya Olasiti Garden leo katika sherehe za siku ya familia ya CRDB ambazo  hufanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na familia za wafnayakazi wa benki pamoja na familia za wateja.  



Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Benki ya CRDB imeendelea kukuza kipato cha familia nyingi nchini za hali ya chini ,kati na juu kwa kuwahimiza wateja wake kufanya uwekezaji wenye tija pamoja na kujiwekea akiba kwa maisha ya baadae.

Hayo yameelezwa Meneja wa Benki ya  CDRB  tawi la Usa lilipo mkoani Arusha  Jenipher  Tond wakati wa maadhimisho ya siku ya Familia ya CRDB iliyofanyika katika viwanja vya Olasiti Garden jijini Arusha na kuzikutanisha familia mbalimbali za wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na familia za wateja wa benki hiyo waishio jijini Arusha.

Meneja huyo amesema kuwa benki hiyo inaendelea kuhamasisha uwekezaji na kutoa mikopo kwa ajili ya kukuza mitaji na kuinua pato la mwananchi mmoja mmoja hadi kwa taifa.

Meneja wa benki hiyo tawi la Meru Leonce Mathey amesema kuwa benki hiyo imesogeza karibu huduma kwa wananchi ikiwemo boda boda ,mama ntilie pamoja na wajasiriamali kwa kuanzisha matawi katika maeneo ya masoko .

Leonce amewataka wafanyakazi wa CRDB kutumia vyema siku familia  kwa kukaa karibu na familia zao na kufurahi pamoja kwani muda mwingi wanautumia katika kufanya kazi za kuwaingizia kipato .

“Kama kwenye familia mambo hayako vizuri nyumbani hata kazini mambo  hayatakua vizuri ni vyema kuhakikisha mazingira yanakua mazuri kuanzia kwenye familia mpaka kazini” Alisema Leons

Kwa upande wake Mteja wa benki hiyo Pendo Shoo amesema kuwa benki hiyo imemsaidia kuwalipia watoto wake ada kupitia akaunti ya Junior Acount ambazo huwawezesha pia kupata mikopo kwa ajili ya kuwaendeleza watoto kielimu.

Benki ya CRDB  ina matawi 8 na matawi mengine madogo madogo bado yataendelea kuanzisha ili kusogeza huduma za kibenki karibu na wananchi.

Siku ya familia ya CRDB iliambatana na michezo   na burudani  ambazo zilipamba siku hiyo ikiwemo mchezo wa kuvuta kamba ,kukimbia na yai mdomoni pamoja na burudani ya muziki .

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...