Pages

November 13, 2015

WADAU WA AFYA MKOANI MBEYA WAKUTANA NA KUJADILIANA KUELEKEA SIKU YA MAADHIMISHO YA UKIMWI DUNIANI


Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa wa Mbeya Ndugu Stellah Kategile akiwasilisha maada kwa wadau wa Sekta ya Afya Mkoani Mbeya katika kikao cha kujadili juu ya kuelekea katika siku ya maadhimisho ya Ukimwi Duniani Tarehe 1 Desemba mwaka huu.
Mratibu wa kudhibiti Ukimwi Mkoani Mbeya (RACC-Regional AIDS Control Coodinator ) Dkt Francis Philly akizungumza katika kikao hicho ambacho kimehudhuriwa na wadau mbalimbali wa masuala ya afya mkoani  katika ukumbi wa Cofee Garden jijini Mbeya.
Mrakibu wa Polisi Mkuu  dawati la jinsi na watoto Mkoa wa mbeya Ndugu Debora Mrema akielezea masuala mbaliimbali  yanayolikumba Dawati hilo katika kupambana na ukatili wa kijinsi Mkoani humo huku akisisitiza juu ya wadau kujitokeza na kutoa michango yao ya kifedha sanjali na rasilimali nyingine ili kuweza kutoa elimu kwa jamii katika maeneo mbalimbali mkoani humo hususani maeneo ya vijijini.
Wadau wakiendelea na majadiliano katika mkutano huo.

Mwakilishi wa Kampuni ya Mbeya Cement jijini Mbeya ambaye ni Mratibu wa Masulaa ya Afya na Jamii Grace Nyatori akichangia katika mkutano hiuo ambao unalenga kujadili na kupitisha bajeti kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani .
Mhariri wa habari kutoka Radio Ushindi jijini Mbeya Edom Mwasamya akizungumza namna ambavyo vituo vya radio vitakavyo weza kuchangia kufanikisha zoezi hilo la siku ya Ukimwi Duniani.
Festo Sikagonamo  kushoto Mkuu wa shirika la Elimisha  pamoja na Neema Stanton Afisa Mahusiano wa Mamlaka ya Maji safi na maji taka jijini hapa wakishirika katika mkutano huo.
Wadau wakiendelea na majadiliano.
Na Emanuel Madafa, JamiimojablogMbeya.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...