Pages

November 13, 2015

UKEKETAJI WAPUNGUA WILAYA YA NGORONGORO


IMG_0842
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii, Teresia Irafay akifungua warsha ya wiki moja ya mafunzo juu ya elimu ya Afya ya Uzazi na Maadili iliyojumuisha wakunga wa Jadi, Waganga wa tiba asili, viongozi wa dini, waandishi wa habari na wahamasishaji afya jamii iliyowaleta pamoja wadau mbalimbali katika ngazi ya vitongoji, vijiji na wilaya kujifunza namna ya kufanya kazi shirikishi ili kuleta mabadiliko katika jamii inayofanyika katika hoteli ya Domel-Wasso, tarafa ya Lolilondo katika wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Mwandishi wetu, Loliondo
IDADI ya wanawake wanaokeketwa Loliondo wilaya ya Ngorongoro imepungua kufikia asilimia 75 kwa mwaka huu.
Hayo yameelezwa na Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto, Loliondo, Bi. Nailejileji Joseph katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii kwenye warsha ya wiki moja ya mafunzo juu ya Elimu ya Afya ya Uzazi na Maadili.
Warsha hiyo inajumuisha wakunga wa Jadi, Waganga wa tiba asili, viongozi wa dini, waandishi wa habari na wahamasishaji afya jamii.

Wadau hao wanatoka ngazi mbalimbali ya vitongoji, vijiji na wilaya.
Lengo la warsha hiyo ni kujifunza namna ya kufanya kazi shirikishi ili kuleta mabadiliko sahihi katika jamii inayofanyika katika hoteli ya Domel-Wasso, tarafa ya Lolilondo katika wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.

Bi Nailejileji alisema idadi ya ukeketaji Loliondo inaonyesha kupungua hadi kufikia 57% mwaka 2015 ikilinganishwa na 87% mwaka 2014 kwa wanawake waliojifungulia hospitalini.

Alisema kwamba matokeo hayo yamefanikiwa kutokana na mkakati maalum unaofanyika shuleni kwa kuanzisha vituo vya kirafiki kwa vijana vinavyolenga kutoa elimu na hamasa kuhusu masuala ya ukeketaji.

Aidha mafanikio hayo ni miongoni mwa jitihada za Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kueneza hamasa shirikishi katika jamii, kuelezea ukubwa wa tatizo, athari zinazotokana na ukeketaji kwa kuwashirikisha wazee wa kimila wa jamii ya Kimasai (Laigwanan) kuchukua hatua zipasazo kukomesha ukatili huu dhidi ya wasichana.
IMG_0843
Wazee wa kimila wa kimasai ni watu wenye kuheshimika na kusikilizwa kwenye jamii pale wanapotoa matamko mbalimbali yanayopelekea kuleta mabadiliko katika jamii ambao wanaonekana kuwa na uwezo mkubwa katika kukomesha ukeketaji na ndoa za utotoni kwa watoto wa kike ambao huozwa baada ya kufanyiwa ukeketaji mwezi Desemba kila mwaka.

Changamoto hizo zinachangiwa kwa kiasi kikubwa na kile kilichoonekana na washiriki kuwa ni mila na tamaduni zilizojengeka katika jamii ya Kimasai kwa vijana kupokea amri kutoka kwa wazazi wao hata kama jambo hilo halina tija katika jamii.

Wakichangia dhana ya mtoto na kijana ni nani, majukumu yao na wana haki gani katika jamii, wadau hao wa jamii ya kimasai walisema kuwa mtoto ni kati ya umri 0-18 na kijana ni yule anayeanzia miaka 18-35.

Wakizungumzia kuhusu haki walisema kwamba mtoto ana haki za kupata huduma muhimu kama kupata elimu, kupata matunzo bora, kuishi kwa usalama au kulindwa, kuwa na afya bora na kuheshimiwa mawazo yake.

Lakini , hata hivyo walisema kwamba, kutokana na tamaduni iliyojengeka miongoni mwa vijana kujifunza na kuiga malezi kutoka kwa wazazi wao, imekuwa ni changamoto kubwa kuhamasisha vizazi kupiga vita mila na desturi  zinazoathiri wanawake.
IMG_0854
Afisa Elimu ya Afya na Ukimwi kutoka Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Mathias Herman akizungumza kwenye warsha ya wiki moja ya mafunzo juu ya Elimu ya Afya ya Uzazi na Maadili iliyojumuisha wakunga wa jadi, waganga wa tiba asili, viongozi wa dini, waandishi wa habari na wahamasishaji afya jamii iliyowaleta pamoja wadau mbalimbali katika ngazi ya vitongoji, vijiji na wilaya kujifunza namna ya kufanya kazi shirikishi ili kuleta mabadiliko katika jamii inayofanyika katika hoteli ya Domel-Wasso, tarafa ya Lolilondo katika wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.

Hata hivyo walisema pamoja na kwamba mabadiliko huchukua muda mrefu, lakini yanaweza kufanikiwa ikiwa wanawake wa kimasai wenyewe watayavalia njuga masuala yanayowahusu katika jamii na yanayohatarisha maisha yao.
 “Ndio mila na tamaduni zipo na kuna msemo unaosema kwamba mkataa kwao ni mtumwa, lakini zipo tamaduni ambazo ni hatarishi na anayeathirika kwa kiasi kikubwa ni wanawake na wasichana,”alisema Nailejileji Joseph.

Mazingira waliyokulia Wanawake wa jamii ya Kimasai yamejenga ukimya miongoni mwao na kuona kwamba changamoto zozote zinazotokea ni jambo la kawaida na hazizungumziki.

Kwa mfano ndoa za utotoni kwa wasichana wa Kimasai ni mwendelezo wa tamaduni hatarishi unaotokana na majukumu ya mtoto au kijana katika jamii ya kupokea anachoamrishwa na wazazi bila kuelewa athari zinazoweza kumpata mtoto wa kike wa jamii hiyo.
IMG_0849
“Mimi nalea mjukuu na binti yangu yaani mama wa huyu mjukuu. Binti yangu amepata ulemavu wa maisha baada ya kujifungua huyu mtoto akiwa na umri wa miaka 13,”alisema Bi. Noorkidemi Kitupei mkazi wa kijiji cha Ilopolum, tarafa ya Loliondo. Binti huyu (jina linahifadhiwa) ni mke wa tatu kuolewa na mume wake akiwa katika umri mdogo baada ya baba yake kuamrisha aolewe.
Changamoto nyingine kama hiyo ilimpata binti mmoja wa kimasai aliyeolewa akiwa na umri wa miaka 13 baada ya kupigwa na kuumizwa mkono na kuachiwa kovu kubwa sana na mumewe baada ya Ngómbe mmoja wa mume wake kupotea, mume wake alichukua jukumu la kumpiga karibia kumpa ulemavu wa mkono baada ya kumuuliza binti huyo kwanini Ngómbe huyo amepotea na kujibiwa kwamba alikuwa amelala.
Kwa mujibu wa Mratibu huyo wa afya ya uzazi visa kama hivyo vinaendelezwa kwa sababu hamasa bado ni ndogo katika jamii ya kimasai na wadau wachache wanaobahatika kupata mafunzo au kwa woga unaotokana na muendelezo wa tamaduni hatarishi zimekuwa hazihamasishwi na haziwafikii walengwa.
Inategemewa kwamba kituo cha redio cha jamii Loliondo FM kitatoa mchango mkubwa wa kuhamasisha jamii masuala mbalimbali ya kijamii na kimaendeleo.
IMG_0856
Mtaalamu wa Masuala ya Vyombo vya Habari Jamii na Mkufunzi kutoka Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu (katikati) akiteta jambo na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii, Teresia Irafay (kulia) wakati warsha hiyo ikiendelea. Kushoto ni Afisa wa UNESCO, Hamidun Kweka.
IMG_0923
Pichani ni mjumuiko wa wakunga wa Jadi, Waganga wa tiba asili, viongozi wa dini, waandishi wa habari na wahamasishaji afya jamii wanaohudhuria warsha hiyo inayoendelea wilayani Ngorongoro.
IMG_0887
IMG_0868
IMG_0892
Afisa Elimu ya Afya na Ukimwi kutoka Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Mathias Herman (wa pili kushoto) akiendesha mafunzo ya uelewa juu ya dhana ya Utamaduni kwa mifano hai katika warsha hiyo ya wiki inayofanyika katika hoteli ya Domel-Wasso, tarafa ya Lolilondo katika wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. Kushoto ni Mshiriki ambaye ni mkalimani wa lugha ya kimasai, Joseph Ndaika na kulia ni wanawake wa kimasai wanaoshiriki warsha hiyo.
IMG_1035
Mtaalamu wa Masuala ya Vyombo vya Habari Jamii na Mkufunzi kutoka Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu (kulia) akifafanua jambo kwa washiriki wakati wa kuhakiki kazi za vikundi katika warsha hiyo inayoendelea wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
IMG_0957
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa kwenye kazi za vikundi.
IMG_0975


--

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...