Pages

November 26, 2015

Sentensi 7 za Mbowe nje ya Mahakama baada ya kuruhusiwa kuaga mwili wa marehemu Mawazo Mwanza.

 
Ishu ya viongozi na wanachama wa CHADEMA kuzuiwa kuaga mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Geita imekuwa ikiripotiwa na kuandikwa kwenye vyombo vya habari huku ikisubiriwa kutolewa majibu na Mahakama Kuu Mwanza kuhusu hatma ya zuio hilo.
Leo maamuzi ya Mahakama Kuu Mwanza yametoka na majibu kwamba wanaCHADEMA na viongozi wao wamepata kibali cha Mahakama hiyo kuendelea na shughuli za kuaga pamoja na mazishi ya kiongozi huyo.
Nje ya Mahakama Kuu Mwanza, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikael Mbowe alipata dakika chache kuongea na wanachama wa CHADEMA ambao walikuwa wakisubiri kusikia maamuzi ya Mahakama >>>> “Ni lazima tukae vikao kupanga ratiba ya kumuaga Kamanda Mawazo, Jaji ametoa maelekezo kwamba viongozi wa CHADEMA, familia ya marehemu na Jeshi la Polisi wakae pamoja kupanga ratiba kamili.”
index-II3
Tutaheshimu maelekezo ya Jaji lakini hatutakubali kuonewa, muwe na imani kwamba haki itatendeka… tunakwenda kwenye vikao lakini tunahitaji kumaliza jambo hili kuanzia kesho, tutamuaga Mawazo kwa heshima anayostahili katika eneo ambalo tutawatangazia.” >>> Freeman Mbowe.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...