Pages

November 12, 2015

NHIF YAWAPIGA MSASA WAKOREA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi wa Mfuko wa bima ya Afya ya Jamii (CHF) Eugen Mikongoti, akizungumza na Wadau wa Maendeleo ya Mfuko wa  Kimataifa wa Afya wa Korea kuhusiana na utekelezaji wa  mifumo ya habari na mawasiliano ya uzalishaji na ufuatiliaji wa madai ya watoa huduma za afya kwa wanachama katika mkutano  uliofanyika  ndani ya Hoteli ya Blue Pearl  Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Mifumo ya Habari wa (NHIF)   Ali Othman akitoa mada katika Mfuko wa  Kimataifa wa Afya wa Korea kuhusu utekelezaji wa  mifumo ya habari na mawasiliano ya uzalishaji na ufatiliaji wa madai ya watoa huduma za afya kwa wanachama katika mkutano  uliofanyika  katika Hoteli ya Blue Pearl  Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya ushirikiano na Maendeleo kutoka Korea, Chun Chang Bae,  akitoa mada katika mkutano wa Maendeleo Mfuko wa  Kimataifa wa Afya wa Korea jijini Dar es Salaam.
 Maofisa wa wa Taifa wa Bima ya Afya  (NHIF) wakiteta jambo kabla ya mkutano  kuanza katika hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam.
 Mkurugezi wa Mfuko wa bima ya Afya ya Jamii (CHF) Eugen Mikongoti, akifafanua jambo mbele ya wandishi wa habari   jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau katika mkutano huo uliofanyika  jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka wa Glub ya jamii

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...