MISS Tanzania 2014, Lilian Kamazima anataraji kuwakilisha
Tanzania katika shindano la Miss World lilipangwa kufanyika Desemba 19 mwaka
huu katika ukumbi wa Beauty Crown Grand Theatre ulipo mji wa Sanya, China.
Shindano hilo la urembo duniani lenye hadhi ya kimataifa
litashirikisha warembo kutoka mataifa 120 toka duniani kote.
Mrembo huyo wa Tanzania pamoja na warembo wengine watakaa katka Hotel
ya Beauty Crown Sanyakatika kambi yao itakayoanza Novemba 21 mwaka huu hadi
siku ya fainali hizo.
Afisa
habari wa kampuni ya Lino International Agency
ambao ndio waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hidan Rico, amesema
Miss Tanzania anataraji kuondoka nchini Novemba 19, kuelekea katika
kambi ya mashindano hayo.
Rico amesema maandalizi ypote muhimu kwaajili ya safari ya mrembo huyo yamekamilika na mrenbo anaendelea kujifua.
"Maandalizi kwaajili ya safari ya mrembo wetu, yamekamilika na kwa sasa anaendea na mazoezi ya kujiweka sawa,"alisema Rico.
Kisiwa cha Sanya China kimekuwa wenyeji wa mashindano ya
urembo ya dunia kwa muda wa miaka mingi tangu mwaka 2005 na mwaka huu pia
washiriki wanatarajia kufurahi na kujiona utajiri na utalii wa China.
Kwa mujibu wa ratiba ya mashindano hayo iliyotolewa na
waandaaji wa shindano hilo, washiriki wote watapata fursa ya kutembela sehemu
mbalimbali ikiwa ni pamoja na sehemu maalum ya ukuta wa China sehemu ambayo
imekuwa kivutio kikubwa kwa watalii
wanaotembelea China.
Washiriki wote wamehamasishwa kutumia Mitandao ya Jamii
kwa madhumuni ya kujitangaza wenyewe na pia kutangaza utalii wa China pamoja na
shindano kubwa lenye hadhi ya kimataifa Shindano la urembo la Dunia.
Mitandao hiyo ya Jamii pia itatoa Alama (Marks) kwa
washiriki wote watakaofanya vizuri katika kutumia Mitandao hiyo, Alama ambazo
pia zitasaidia katika kuongeza nafasi za ushindi katika shindano hilo.
Afisa habari wa kampuni ya Lino International Agency
ambao ndio waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hidan Rico amesema hii ni
fursa pekee kwa watanzania kumpa ushindi mrembo wao.
“Tunawaomba Watanzania kutembelea Mitandao hiyo ya mrembo wetu wa Tanzania, facebook pamoja na
twitter ili kumpa sapoti na kumuongezea Alama mrembo wetu,”alisema Rico.
Tunawaomba pia Watanzania wote wanaoishi hapa nchini
pamoja na wale wa Nchi za nje wenye uwezo kuhudhuria Fainali za Shindano la
urembo la Dunia litakalofanyika tarehe 19 Desemba 2015 katika ukumbi wa Beauty
Crown Grand Theatre uliopo Sanya china.
No comments:
Post a Comment