Pages

November 30, 2015

Baada ya kipigo cha West Brom, Arsenal walazimishwa sare na Norwich City, Full Time ya EPL Nov 29

Mtu wangu mpenda soka najua ungependa kufahamu matokeo ya muendelezo wa mechi nne za Ligi Kuu Uingereza zilizochezwa Jumapili ya November 29.Zilipigwa mechi nne tu za Ligi Kuu Uingereza miongoni mwa mechi zilizopigwa November 29 ni mechi kati ya Norwich City dhidi ya Arsenal katika dimba la Carrow Road.
2725
Arsenal waliingia uwanjani wakiwa wanacheza mechi yao ya pili mfululizo ugenini, baada ya wiki iliyopita kukubali kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa West Brom, mchezo uliochezwa katika dimba la The Hawthorns lenye uwezo wa kuchukua zaidi ya mashabiki 26,000, kabla ya November 29 Arsenal kulazimishwa sare ya goli 1-1 na Norwich City na weekend iliyopita kupokea kipigo.
3575
Licha ya kuwa Arsenal walikuwa mahiri uwanjani kwa kufanikiwa kumiliki mpira kwa asilimia 63 na Norwich City asilimia 37, walishindwa kulinda goli lao lililofungwa na Mesut Ozil dakika ya 30 kipindi cha kwanza na Norwich City walifanikiwa kusawazisha goli hilo dakika ya 43 kupitia kwa Lewis Grabban.
3648
Matokeo ya mechi za Ligi Kuu Uingereza zilizochezwa November 29
  • Tottenham Hotspur 0 – 0 Chelsea
  • West Ham United 1 – 1 West Bromwich Albion
  • Liverpool 1 – 0 Swansea City
Video ya magoli ya mechi kati ya Norwich City Vs Arsenal

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...