Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi katika Mahakama kama ifuatavyo;
Rais amemteua Bi. Katarina Revocati kuwa
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania (Chief Registrar). Kabla ya uteuzi
huu, Bi. Revocati alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani.
Rais pia amemteua Ndugu John Rugalema
Kahyoza kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani na kabla ya uteuzi huu, Ndugu
Kahyoza alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu.
Mwingine aliyeteuliwa ni Ndugu Ilvin
Claud Mugeta ambaye anakuwa Msajili wa Mahakama Kuu. Kabla ya Uteuzi huu
ndugu Mugeta alikua Mkurugenzi wa Ukaguzi na Maadili.
Uteuzi huu umeanza tarehe 3 Oktoba,2015.

Post a Comment