Baadhi
ya vijana hao wakiwa darasani wakifurahia masomo wanayopatiwa ya
kujiandaa na elimu ya sekondari katika kituo hicho cha Furahini mkoani
Kilimanjaro.
Na Mwandishi wetu
TAASISI
ya misaada ya Mo Dewji Foundation imekubali kufadhili mradi wa kituo
cha mafunzo cha vijana cha Furahini (FYLC) wenye lengo la kuboresha
upatikanaji wa elimu katika kijiji cha Kisangara mkoani Kilimanjaro.
Imeelezwa
kuwa taasisi hiyo ya bilionea Mo Dewji imetoa shilingi milioni 7
kusaidia ujenzi wa miundombinu inayotakiwa na kituo hicho chenye lengo
la kuboresha elimu kwa watoto wa kijiji hicho.
Baadhi ya watoto hao ni wawafanyakazi wa mashamba ya Mkonge ya MeTL yaliyopo jirani na kijiji hicho.
Ufadhili
huo unaenda sambamba na sera za MeTL za urejeshaji wa faida yake kwa
wananchi kama sehemu ya wajibu wake kwa jamii, wenye lengo la kuimarisha
ustawi wa jamii inayochangia biashara za kampuni hiyo.
Taasisi
ya Mo Dewji ambayo ndiyo inatekeleza wajibu wa kundi la makampuni ya
MeTL la kurejesha faida kwa umma, kwa ufadhili huo kwa kikundi cha
Furahini wametanua wigo kutoka katika shughuli mbalimbaliw alizokuwa
wakufadhili mkoani Singida.
Lengo la ufadhili huo ni kuwezesha jamii yenye kipato cha chini kabisa kuweza kumudu mikiki ya elimu ili kukabili umaskini.
Toka
mwaka 2000 kundi la makampuni ya MeTL imekuwa ikitanua mazingira ya
urejeshaji wa faida kwa umma kutokana na shughuli zake mbalimbali.
Katika kipindi cha miaka mitano taasisi ya Mo Dewji imetumia zaidi ya
dola za Marekani milioni 3 kusaidia miradi mbalimbali ya jamii.
Baadhi
ya vijana hao wakiwa darasani wakiendelea na masomo katika jengo la
kituo hicho cha Furahini ambacho kinatarajiwa kukabaratiwa na kwa msaada
wa Mo Dewji Foundation.
Tangu
kuanzishwa kwa Taasisi hiyo, shughuli mbalimbali zimedhaminiwa na
kufadhiliwa. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule, uchimbaji wa
visima, ugawaji wa vyandarua, usambazaji wa unga wa mahindi kwa wananchi
waliokumbwa na baa la ukame kwa mwaka 2005-2006,ufadhili kwa wanafunzi
wa sekondari,afya kw awale waliozidiwa kiafya, kujenga kitengo cha macho
katika hospitali za mkoa,kuweka taa katika mitaa, msaada wa chakula kwa
waliokumbwa na ugonjwa wa ukimwi, ununuzi wa vifaa vya michezo na vifaa
vya wakulima.
Kwa
mujibu wa mratibu wa kituo hicho cha Furahini (FYLC) Bw. Msuya Isiaka,
wazo la kuanzishwa kwa kituo lilitokana na uzoefu wa muda mrefu wa
ufundishaji katika eneo hilo la mahusiano ya jamii.
Alisema
wazo la kuanzishwa kwa kituo limetokana hasa na matokeo mabaya ya
mitihani kwa wanafunzi wanoasoma shule za umma katika kijiji hicho.
“Elimu
imekuwa tatizo kubwa katika jamii yetu hasa katika shule za serikali
ambazo mara nyingi zimejikuta hazina walimu, na kama wakiwa wamebahatika
wanakuwa na mwalimu mmoja wa somo la hisabati kwa shule nzima, bila
kutaja masomo mengine kama fizikia, kemia na bayolojia,” alisema Isiaka
na kuongeza kwamba kuna shida kubwa ya uwajibikaji kwa wlaimu na hivyo
kluleta athari mbaya kwa wanafunzi.
“Tunaamini
kwamba silaha yetu kubwa ya kukabili umaskini unaozunguka katika vizazi
vyetu hapa Kisangara ni kuwa na elimu bora” alisema.
Kwa mujibu wa Isiaka kituo hicho kinatakiwa kuwa na maktaba kamili na chumba cha tehama.
“Kwa
kuwa na miundombinu hiyo ya kujifunzia ya maktaba na tehama, wanafunzi
wanakuwa katika nafasi ya kujifunza vyema na kuwa katika hali ya
kukabili umaskini unaozunguka janmii yetu.” alisema.
Mratibu huyo alisema kwamba mafunzo katika kituo hicho katika masomo ya kemia,fizikia,bayolojia na hisabati yalianza Juni 2015.
Kituo
cha Furahini ambacho kimejengwa katika ardhi yenye ukubwa wa nusu eka
katika kijiji cha Kisangara kata ya Mtuva katika wilaya ya Mwanga mkoani
Kilimanjarokipo umbali wa kilometa 2.5 kutoka kituo cha mabasi cha
Kisangara.
Kijiji
cha Kisangara ambacho kipo katika eneo kame wastani kina wakazi wa
kutoka makabila mbalimbali ambayo yalifika hapo kufanyakazi katika
mashamba ya mkonge.
Mkonge ndio zao kubwa la biashara ambalo linalimwa na kampuni ya MeTL ikiajiri idadi kubwa ya watu kutoka katika kijiji hicho.
Eneo la jengo hilo la kituo linavyoonekana kwa nje.
Ukame
uliitafuta Kisangara kwa muda mrefu umesababisha kasi kubwa ya
umaskini. Kutokana na hali hiyo watoto wameathirika zaidi kutokana na
familia zao kushindwa kuwapeleka shule binafsi na kuwaacha katika shule
za umma ambazo hazina ubora.
Kutokana
na hali hiyo FYLC inajipanga kuhakikisha kwamba inarejesha matumaini
kwa kuwawezesha wanafunzi hao kupunguza tofauti kati ya wanafunziw
aosoma shule binafsi na shule za umma katika masomo.
Kituo
kikiwa na wanafunzi 86 wa umri kati ya miaka 13 hadi 14 wanafundishwa
kujiandaa kuingia kidtao cha kwanza kwa kufunzwa Fizikia,
kemia,bayolojia,jiografia na Kiingereza.
Lengo
kuu la kituo ni kuhakikisha kwamba wanawawezesha wanafunzi wanaosoma
shule za umma wanakuwa na uwezo mkubwa kwa kuwapa nafasi ya kutumia
maktaba na chumba cha Tehama na kuwapelekea walimu waliobobea kuwanoa
wanafunzi hao na kuleta mabadiliko.
Aidha kituo kitatoa elimu ya maarifa ya afya ya uzazi kwa vijana ili kuweza kubadili maisha yao na kuondokana na tabia mbaya.
Ukarabati wa kituo hicho ukianza baada ya Mo Dewji Foundation kukipiga tafu.
Mratibu
wa Furahini Youth Learning Centre, Isiaka Msuya katika zoezi la kupakia
matofali kwa ajili ya ukarabati wa kituo hicho kwa msaada wa Mo Dewji
Foundation.
No comments:
Post a Comment