Balozi
Mwapachu (kulia) akikabidhi kadi yake ya uanachama wa CCM kwa Katibu wa
Siasa na Uenezi CCM, mtaa wa Mikocheni A, Sudi Odemba.
KADA
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EAC), Balozi Juma Mwapachu leo amerejesha kadi yake
ya uanachama ofisi za chama hicho zilizopo Mikocheni A jijini Dar es
Salaam.
Balozi
Mwapachu aliyetangaza kukihama chama hicho juzi (Jumanne) kwa madai
kuwa kimepoteza dira, amekabidhi kadi hiyo kwa Katibu wa Siasa na Uenezi
CCM, mtaa wa Mikocheni A, Sudi Odemba.
Mwanasiasa huyo ambaye amekuwa ndani ya CCM kwa miaka 48 alisema bado hajaamua ahamie chama gani.



Post a Comment