Na John Gagarini, Lugoba
Wagombea
wa nafasi za uongozi hapa nchini wametakiwa kukubali matokeo mara
uchaguzi utakapofanyika Oktoba 25 mwaka huu kwani kuna maisha mengine
baada ya uchaguzi, na kuendelea kufanya kampeni zao huku wakiendelea
kuhubiri na kulinda amani iliyopo kwani wana nafasi kubwa ya
kuwashawishi wafuasi wao wasifanye vurugu au kufanya vitendo
vinavyosababisha uvunjifu wa amani.
Pia
wagombea watakaoshindwa kwenye uchaguzi mkuu wameombwa wakubali matokeo
kwani kwenye washindani lazima kuwe na washindwa ili kuondoa hali ya
mafarakano kwani kwa wale watakaoshindwa wasipokubali matokeo wanaweza
kuleta uvunjifu wa amani.
Hayo
yalisemwa katika Kijiji cha Maviayangombe kata ya Lugoba wilayani
Bagamoyo mkoani
Pwani na Askofu mkuu wa Dayosisi ya Morogoro ya Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT) Jacob Mameo Ole Paulo wa Dayosisi ya Morogoro
wakati wa mazishi ya mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa wafugaji Laban
Moreto, Karokya Moreto (33) ambaye alikuwa mwanajeshi wa kikosi cha
04/691 cha Mtwara.
Askofu
Ole Paulo alisema kuwa wagombea hao wanauwezo wa kudumisha amani kwa
kuhubiri au kuingiza nchi kwenye machafuko endapo watayatumia vibaya
majukwaa wakati wa kipindi hichi cha kampeni za uchaguzi.
“Wanapaswa
kuhubiri amani na kuacha kutumia maneno yatakayo haribu amani ya nchi
iliyopo ambayo imedumu kwa kipindi kirefu tangu nchi ilipopata uhuru
miaka zaidi ya 50 hivyo itakuwa ajabu ivunjwe kisa kuwania uongozi tu,”
alisema Askofu Ole Paulo.
Alisisitiza
kuwa vyama vya siasa vinapaswa kupingana kwa hoja na kwa malumbano
ambayo hayana maana bali yanaweza kuleta mitafaruku isiyokuwa ya lazima
hasa kwa wale wanaoshindwa kwani wanapaswa kukubali matokeo.
Kwa
upande wake Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete alisema kuwa
amesikitishwa na kifo cha marehemu ambaye alikuwa ni ndugu kwani
wamekuwa wakiishi kama familia moja na walikuwa na ushirikiano mkubwa
baina ya familia zao.
Ridhiwani
alisema kuwa kifo hicho ni pigo kwa familia hiyo pia kwa Taifa kwani
alikuwa ni mtumishi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na alikuwa
mtaalamu wa rada hivyo pengo lake haliwezi kuzibika kikubwa ni kumwombea
marehemu.
Rais
Dk Jakaya Kikwete alituma salamu za pole kwa familia hiyo kupitia kwa
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete na kusema kuwa anatoa pole
na Mungu awape nguvu katika kipindi hichi kigumu cha maombolezo na yuko
pamoja nao.
Alisema
kuwa Rais alishindwa kuhudhuria msiba huo kwani kwa sasa yuko nje ya
nchi lakini pindi atakaporudi ataitembelea familia hiyo kwa ajili ya
kuifariji kufuatia kifo cha mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa kabila
wafugaji
Naye
mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) Mathayo Torongei alisema ili amani iendelee kuwepo
ni vema dola ikatenda haki badala ya kupendelea upande mmoja.
Marehemu
alifariki kwa ajali baada ya gari alilokuwa akiendesha kupasuka tairi
la mbele na kusababisha ajali iliyopelekea kifo chake siku ya Septemba
16 mwaka huu huko Mtwara. Ameacha mke na watoto watatu.
Baadhi ya akinamama ambao ni ndugu wakaribu wakilia
Jeneza lenye mwili wa marehemu likiwa limebebwa na wanajeshi ukiwasili makaburini
Baadhi ya Wazee wakiwa wamekaa kwenye msiba huo huko kijiji cha Maviyangombe Lugoba wilayani Bagamoyo.
Kulia
ni Ridhiwani Kikwete mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM
akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga, mkuu wa wilaya ya
Nachingwea Pololet Mgema na mgombea ubunge Jimbo hilo kupitia Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Matayo Torongei wakiwa kwenye msiba
huo.
Askofu Jacob Mameo Ole Paulo akizungumza wakati wa msiba huo.
No comments:
Post a Comment