Pages

September 25, 2015

WAIMBAJI NYIMBO ZA INJILI WAAOMBA WATANZANIA KUJITOKEZA KATIKA TAMASHA LA KUOMBEA AMANI


 Mwimbaji  wa nyimbo za Injili Upendo Nkone (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  katika ofisi za  Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha kuombea amani ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama  kuhusiana na kushiriki katika tamasha la kuombea amani kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu. Kulia ni Mwimbaji wa nyimbo za Injili John Lisu na kustoto ni Christophe Mwanganyira.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili John Lisu akizungumza leo jijini Dar es Salaam jinsi tamasha la kuombea Amani ambapo wasanii hao watakavyo tumbuiza katika tamasha hilolitakalofanyika jijini Dar es Salaam katika uwanja wa taifa. Mwimbaji  wa nyimbo za Injili Upendo Nkone (katikati) naMwimbaji wa nyimbo za Injili John Lisu na kustoto ni Christophe Mwanganyira. 
Kutoka kulia ni Mwimbaji wa nyimbo za Injili  Mathar Mwaipaja akizungumza na waandishi wa habari kuwa watu wote wajitokeze katika Tamasha hilo la kuombea amani na kuwa viingilio vyake kuwa sio vikubwa sana kwa watu wazima ni shilingi elfu tatu na watoto shilingi elfu moja pamoja na VIP  ni shilingi elfu tano.
Baadhi ya waandishi waliohudhulia katika katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
WASANII wa nyimbo za Injili wajitokeza katika  kuzungumzia Tamasha  la kuombea amani litakalofanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es  Salaam Oktoba 4 Mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama amesema wamejiandaa vizuli katika ulinzi pamoja na vyombo vya mziki vitakavyo tumika kutumbuizia siku hiyo.
Pia amesema kuwa watanzania wajitokeze kwa wingi katika ufanikishaji wa tamasha hilo ambalo linatakiwa kuwa na tamko moja la amani kuelekea uchaguzi mkuu ambao utahusisha nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais,” alisema Msama.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...