Afisa
Mawasiliano wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Fausta Msokwa
akiongea na waandishi wa habari mapema leo asubuhi jijini Dar es
Salaam juu ya maadhimisho ya miaka nane ya mafanikio ya TMF. Pembeni ni
Mkurugenzi wa TMF, Ernest Sungura na Afisa Mafunzo wa TMF, Radhia
Mwawanga.
Mkurugenzi
wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Ernest Sungura akiongea
kwenye mkutano na waandishi wa habari kutangaza tukio hilo, alisema
Tarehe 22 Septemba, 2015 tutakuwa na tukio la madhimisho ambayo
yatajumuisha maonyesho kwa ajili ya waandishi wa habari waliowezeshwa
na misaada ya TMF kuonyesha kazi zao na jinsi gani zimechangia kuleta
uwajibikaji na pia kuonyesha kazi ambazo zimepandisha kiwango cha
mijadala ya umma katika masuala husika hususani utawala bora na haki
za binadamu pamoja na sherehe ya utoaji tuzo kwa waandishi
waliowezeshwa na TMF na kazi zao kuweza kuleta mabadiliko chanya.
Waandishi
wa habari wakichukua tukio.
---
Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) utaadhimisha miaka nane ya
mafanikio katika kuongeza uwajibikaji kwa kuimarisha sekta ya habari
nchini Tanzania kupitia tukio ambalo litafanyika jijini Dar es salaam.
Tukio
hilo litawaleta pamoja waandishi wa habari na wanataaluma wengine ambao
wamewezeshwa na misaada ya TMF, wafadhili, wadau wa sekta ya habari
pamoja na taasisi za kiraia na serikali.
Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari kutangaza tukio hilo,
Mkurugenzi wa TMF, Ernest Sungura alisema:
“Tarehe 22 Septemba, 2015 tutakuwa na tukio la madhimisho ambayo
yatajumuisha maonyesho kwa ajili ya waandishi wa habari waliowezeshwa na
misaada ya TMF kuonyesha kazi zao na jinsi gani zimechangia kuleta
uwajibikaji na pia kuonyesha kazi ambazo zimepandisha kiwango cha
mijadala ya umma katika masuala husika hususani utawala bora na haki za
binadamu pamoja na sherehe ya utoaji tuzo kwa waandishi waliowezeshwa
na TMF na kazi zao kuweza kuleta mabadiliko chanya.
Vile
vile kutakuwa na mjadala utakaohusisha wataalamu wa habari na
wanaharakati kutoka asasi za kiraia katika kujadili changamoto
mbalimbali kama vile kuwajengea uwezo wanahabari na pia kuweka mazingira
endelevu na uhuru wa habari.
Sasa
ni miaka nane tangu TMF ilipoanzishwa na tumetoka mbali. Maadhimisho
haya yatatupatia fursa ya kutafakari kwa pamoja tulipotoka, mambo
tuliyoyafanya na pia tutapeana changamoto kufikiri zaidi jinsi ambavyo
sekta ya habari nchini Tanzania inaweza kubadilishwa ili kukuza
uwajibikaji.”
Tangu ilipoanzishwa mwaka 2008, TMF imetoa misaada na kuwawezesha
waandishi wa habari zaidi ya 570 na zaidi ya taasisi za habari 120.
Katika kipindi hiki, TMF imehusika na kuunga mkono jitihada za wadau
wengine wa habari na asasi za kiraia katika kukuza uhuru wa habari.
Mtandao wa TMF umevuka jiji la Dar es salaam na kufikia pembe zote za
nchi na unawagusa viongozi waandamizi wa vyombo vya habari pamoja na
waandishi waliopo maeneo yote ya nchi.
Uchambuzi wa TMF kuhusu taarifa mbalimbali zinazotolewa na vyombo vya
habari unaonyesha kwamba habari ambazo zimefadhiliwa na TMF zimegusa
masuala ya vijijini kwa kiwango kikubwa. Asilimia 82 ya misaada ya TMF
uelekezwa ukilinganisha na asilimia 25 iliyoelekezwa kwenye habari za
mijini.
Vilevile
uchambuzi umeonyesha kwamba taarifa zilizofadhiliwa na TMF huwa na
ubora wa hali ya juu ukilinganisha na taarifa za kawaida zinazoandikwa
au kutangazwa na vyombo vya habari nchini.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa TMF, maadhimisho hayo pia yatatumika
kuzindua Tanzania Media Foundation, taasisi mpya ambayo itachukua nafasi
ya Tanzania Media Fund ambao ni mradi ulioanzishwa na wafadhili.
“TMF
mpya itakuwa ni mpango ulioanzishwa na Watanzania na kufanya kazi
katika misingi ile ile kama mradi wa TMF lakini itaelekeza nguvu zaidi
katika kuhakikisha yanakuwepo mazingira endelevu kwa ajili ya ukuaji wa
TMF pamoja na wanahabari wanaosaidiwa na TMF.
Tutaanzisha
upya mpango wa kuwezesha upatikanaji wa habari ambazo zina maslahi
makubwa ya taifa.
Tutafanya kazi na wazalishaji vipindi ili kuongeza habari za ndani ili
kuvisaidia vituo vya televisheni kutimiza wajibu wa kisheria kama
ilivyoagizwa na TCRA ya kuwa na vipindi asilimia 60 vinavyohusu masuala
ya ndani.
Tunataka
kuhakikisha vituo vya habari vinatoa habari za kukidhi mahitaji
mbalimbali.”
"Tanzania Media Foundation itaanza kazi kwa kukutana na wadau mbalimbali
wa habari nchi nzima na itafanya nao kazi ili kutambua habari ambazo
zitaleta mabadiliko chanya katika jamii.”
No comments:
Post a Comment