Habari
zilizotufikia jioni hii zinasema kwamba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Ompeshi Kombani (pichani),
amefariki dunia huko India alikokuwa akipata matibabu ya saratani.
Alikuwa na umri wa miaka 56.
Taarifa
kutoka ofisi za Bunge zimethibitisha kifo hicho na kueleza kwamba mwili
wa marehemu unategemewa kuwasili Dar es salaam siku ya Jumatatu, ambapo
Bunge na Serikali zitasimamia maandalizi yote ya maziko na kumsafirisha
kwa mazishi nyumbani kwa marehemu huko Mahenge ambako alikuwa Mbunge wa
jimbo la Ulanga Mashariki.
No comments:
Post a Comment