Mwaka 2013 Mario Sergio Machado Nunes, ambaye ni mmoja wa wauzaji wakubwa wa dawa za kulevya Brazil aliwazidi ujanja polisi na kutoroka gerezani.
Baada ya kutoroka gerezani aliamua
kwenda kufanyiwa upasuaji na kubadilisha umbo lake huku akitumia
vitambulisho feki ili asiweze kukamatwa.
Headlines za sasa ni kwamba Polisi
wa nchini hiyo wamemtia mikononi mtuhumiwa huyo na sasa yupo chini ya
ulinzi mkali baada ya kumkamata akiwa katika jumba moja la kifahari
katika mji wa pwani wa Guajura.
Sergio maarufu kama “O Goiano”
amekuwa akisafirisha madawa ya kulevya kati ya Marekani Kusini na
Afrika akishirikiana na mlanguzi maarufu wa madawa ya kulevya raia wa
Colombia Pablo Escobar.
No comments:
Post a Comment