Pages

August 7, 2015

WANAFUNZI NA WANANCHI WAFURAHIA BANDA LA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA(ATC)NANE NANE ARUSHA

Wanafunzi na wananchi wakipata maelezo kwenye banda la Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)juu ya matumizi ya nishati ya Nguvu jua.

Wananchi wanaotembelea maonesho ya Kilimo na mifugo Nananane Njiro jijini Arusha wakiwa kwenye banda la Chuo cha Ufundi Arusha kupata maelezo ya namna kinavyotimiza wajibu wake kuelimisha vijana katika taaluma ya ufundi nchini.

Wanafunzi na wananchi wakipata maelezo kutoka kwa Mkufunzi wa Mitambo,Frank Moshi kwenye banda la Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)juu ya matumizi ya nishati ya Nguvu jua .

ATC pia hutoa mafunzo ya kuongeza thamani madini  hapa nchini badala ya kusafirishwa yakiwa ghafi kwa kuchakata katika mwonekano unaongeza thamani na kuongeza ajira kwa vijana.

Mkufunzi wa Maabara Lemael Anael wa  ATC akimpa maelezo mmoja wa wananchi waliofika kujifunza,Chuo hicho hutoa mafunzo kwa walimu wa maabara katika Shule za Sekondari nchini katika masomo ya Fizikia,Kemia na Bailojia. 


Wanafunzi wa shule za Sekondari wakijifunza mambo mbalimbali katika maonesho hayo.
Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...