Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Chama cha Walimu mkoa wa Arusha CWT
wamelalamikia serikali na kuitaka kutekeleza kwa wakati madeni yao la zaidi ya
billioni 4 kwani yamekuwa kikwazo katika ufanisi wa kazi hali ambayo inapelekea
walimu wengi kushindwa kuendelea kufanya kazi kwa moyo na kujituma jambo ambalo
linaweza kushusha kiwango cha elimu nchini.
Akizungumza na Waandishi wa habari,
Mwenyekiti wa chama cha walimu mkoa wa Arusha Mwalimu Juvin Kuyenga amesema,
kumekuwa na chanagamoto kubwa ambazo zinakwamisha ufanisi wa kazi kwa walimu
kwani wanazidai halmashauri zilizopo mkoani zarusha zaidi ya billioni nne
,amabapo katika jiji la arusha wanadai millioni 987,689,00,Arumeru
billioni 2,996,607,848.21,Karatu millioni 423,983,820,Longido millioni
171,112,680, Ngorongoro million 169,000,000, na Monduli 135,832,000.
Mwalimu Kuyenga ameendelea kusema
kuwa,madeni haya yanatokana na madai mbalimbali ikiwa ni pamoja na malimbikizo
ya mishahara ,mafunzo,uhamisho,matibabu na likizo pamoja na mapunjo ya mshahara
na madeni haya yamekuwa ni kero kubwa na
kusababisha wakati mwingine walimu kuzichukia kazi zao.
Alisema kuwa Walimu wamekuwa wakigota
madaraja bila kupanda kwa muda mrefu kati ya walimu 12,319 waliopo mkoani
arusha walimu 5,364 wamegota kwenye madaraja yao na bado hawajafunguliwa
pamoja na serikali ilishatoa waraka wa kufungua madaraja tangu julai 2014 hivyo
wametaka seriakali kuhakikisha inapandisha madaraja kwa wakati.
‘Posho ya madaraka kwa viongozi wa
elimu, wakuu wa shule,wakuu wa vyuo kutokana na waraka wa seriakali uliotolewa
mwaka jana posho hiyo alitakiwa ianze kutolewa kuanzia julai mwaka huu 2015
lakini hadi sasa bado pesa hiyo haijanza kutolewa hii inakuwa kama danganya toto
kwa viongozi wetu” alisema mwalimu Juvin Kuyenga.
Hivyo wameilalamikia serikali juu ya kuchelewesha
kwa malipo kwa wastaafu, sababu kuna walimuwaliostaafu toka january zaidi
ya walimu 67 huku wakiishi katika mateso ilihali wameshastaafu kazi na mpaka
leo hawajapata viiinua mgongo vyao
“Tunaidai serikali sababu
tunapowasiliana na hawa wa mifuko ya hifadhi za jamii inasema serikali
bado haijawarejesha michango ya walimu inayotakiwa kupelekwa hivyo na danadana
hizi zinawafanya walimu kuona haki zao zinanyonywa kwani utasababisha ufanisi
kuwa mdogo makazini” Alisema
Sababui swala hili laweza kupelekea
malumbano kati ya walimu na serikali ukizingatia katika kipindi cha kueleka
katika uchaguzi ,mitihani ya darasa la saba na kidato cha nne kwani kukataa
huku tamaa kunaweza kupelekea vitu hivyo vya taifa kushindwa kufanikiwa.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha
Walimu mkoa wa Arusha, Mwalimu Hassan Saidi amesema chama hicho kimetoa wiki
mbili kwa waajiri wa halmashauri zilizopo mkoa wa arusha kuwarudisha
majumbani walimu waliostaafu na wanaostaafu na wasipofanya hivyo watawachukulia
hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwashtaki mahakamani kwani wamekuwa wakiteseka
sana baada ya kustaafu na ni kinyume cha sheria .
Mwalimu Saidi , amewataka wagombea
wa Uraisi kutazama vipaumbele vya walimu walivyovitoa likiwemo la kuwapatia
walimu kompyuta mpakato (laptop) wakati wanamahitaji mengi na ya msingi
zaidi ya hayo ikiwa ni pamoja na mishahara isiyokidhi mahitaji ya walimu na
kurejeshwa na kwa posho ya kufundishia kwa walimu.
No comments:
Post a Comment