Pages

August 18, 2015

TAMASHA LA 10 LA VYOMBO VYA HABARI KUFANYIKA SHEIKH AMRI ABEID

Mwandishi wetu, Arusha
Tamasha la 10 la vyombo vya habari  na wadau wa habari mkoa wa Arusha, linatarajiwa kufanyika Agosti 29 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa kushirikisha timu nane ikiwepo  timu ya TASWA kutoka jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Palace Hotel jana, Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo mkoa wa Arusha(TASWA-Arusha), Mussa Juma, alisema tayari maandalizi muhimu yamekamilika.
Juma alisema Tamasha hilo linaloandaliwa na TASWA na kampuni ya Arusha Media.mdhamini Mkuu ni Kampuni ya Bia nchini( TBL) kwa miaka 10 sasa, litashirikisha michezo ya Soka, Mpira wa pete, kuvuta kamba na kukimbiza kuku.
"tunapenda kutangaza rasmi tamasha la 10 ya TASWA Arusha litafanyika Agosti 29 na kauli mbiu yetu ni Uchaguzi Mkuu bila vurugu inawezekana"alisema
Alisema katika Tamasha hilo, ambalo litashirikisha pia timu za wafanyakazi wa kampuni ya bia nchini(TBL) Taasisi na Faidika na kampuni ya Pepsi litaandamana na ziara ya wanahabari kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Arusha.
 
Wakizungumza katika kikao hicho, Meneja wa Masoko wa kampuni ya Mega Trade Edmund Rutaraka, Meneja masoko wa kampuni ya SBC(T) Lalit Sharma na Meneja wa Faidika Arusha,Eliya Mlay walisema wamedhamini Tamasha hilo ili kuendeleza michezo.
Rutaraka alisema kampuni yao kwa miaka mitano sasa inadhamini tamasha hilo na wanajivunia mafanikio makubwa.
Tamasha hilo, limedhaminiwa na kampuni ya bia nchini(TBL) Kampuni ya Mega Trade,Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA),Shirika la Nyumba nchini (NHC) Kampuni ya SBC(T) Ltd,Mamlaka hifadhi Ngorongoro(NCAA), Taasisi ya FAIDIKA na Tanzanite One.
Makamu Mwenyekiti wa TASWA Arusha, Adrea Ngobole alisema wadhamini wengine wa Tamasha hilo watatangazwa karibuni sambamba na zawadi na mgeni rasmi.

Meneja wa masoko na mauzo wa Kampuni ya SBC(T) Lalit Sharma, akimkabidhi mipira Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani mkoa wa Arusha, Mussa Juma kwa ajili ya Tamasha la kumi la waandishi wa habari mkoa wa Arusha,Manyara na Dar es Salaam na wadau wa habari, ambalo litafanyika Agoust 29 uwanja wa Sheikh Amri Abeid.


Meneja masoko na mauzo wa Kampuni ya Mega Trade  Edmundi Rutaraka, akimkabidhi hundi ya Ts 1.5 Milioni Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani mkoa wa Arusha,Mussa Juma kwa ajili ya tamasha la  10 waandishi wa habari mkoa wa Arusha, Manyara na Dar es salam na wadau wa habari ambalo litafanyika Agoust 29 uwanja wa sheikh Amri Abeid, hafla hiyo ilifanyika jana, Palace Hoteli Jijini Arusha.

Makamu Mwenyekiti wa TASWA mkoa wa Arusha,Andrea Ngobole, akipokea  vikombe kutoka kwa Filbert Masele meneja mikopo ya wafanyakazi wa FAIDIKA na Meneja wa FAIDIKA mkoa wa Arusha Eliya Mlay jana Palace Hotel  kwa ajili ya tamasha la waandishi wa habari na ambalo litashirikisha pia wafanyakazi wa taasisi hiyo, ambalo litafanyika Augost 29 uwanja wa Sheikh Amri Abeid

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...