Pages

August 6, 2015

Msaada wa kisheria bila ya malipo Shehia ya Mchangamdogo

 MZEE mmoja ambae hakupatikana jina lake, kutoka shehia ya Mchanga mdogo wilaya ya Wete Pemba, akiuliza suali juu ya umiliki wa ardhi, kwa watendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, wakati walipofika shehiani hapo, kutoa msaada wa kisheri bila ya malipo, wakiambatana na wanasheria wengine, (Picha na Haji Nassor, Pemba)
 MWANASHERIA kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka ‘DPP’ kisiwani Pemba, Seif Mohamed Khamis akijibu masualia mbali mbali hasa ya usalama barabarani, yalioulizwa kwa wananchi wa shehia ya Mchanga mdogo wilaya ya Wete, wakati watendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, tawi la Pemba, walipofika kijijini hapo kutoa msaada wa kisheria bila ya malipo, (picha na Haji Nassor, Pemba).
 AFISA Mipango wa Kituo cha Huduma za sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, mwalimu Mohamed Hassan Ali, akifafanua jambo kwenye mkutano wa wazi ulioandaliwa na ‘ZLSC’ wa kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi wa shehia ya Mchanga mdogo wilaya ya Wete Pemba bila ya malipo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WANANCHI wa Mchanga mdogo wilaya ya Wete Pemba, wakisoma majarida maalumu yanayochapishwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, majarida hayo yaligawiwa wakati watendaji wa ZLSC, walipofika shehiani hapo, kutoa msaada wa kisheria bila ya malipo ikiwa ni ziara yao kwa wilaya nne za Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...