Walinzi wa pwani wa Utaliano wanasema kuwa wanaongoza shughuli za kuwaokoa wahamiaji kama elfu-tatu hivi ambao wametuma ishara ya kuwa taabani kwenye mashua nje ya pwani ya Libya. Mashua kadha zinashiriki katika uokozi.
Bahari baina ya Libya na Utaliano, ndio njia inayotumiwa kwa muda mrefu, na wakimbizi kutoka Afrika na Mashariki ya Kati, ili kuingia Ulaya.
Kati ya wahamiaji 264,500 Umoja wa mataifa unasema kuwa bahari ya Mediterranea ndio kivukio maarufu.Kufikia sasa takriban watu laki moja wamewasili katika ufukwe wa Italia
Wengine zaidi ya laki moja u nusu 160,000 waliwasili Ugiriki.
Jarida moja la Norway Aftenposten, limesema kuwa manuari ya kijeshi ya taifa hilo Siem Pilot, liko njiani kuwasaidia wahamiaji hao walioko mashakani.
Manuari hiyo iliwaokoa wahamiaji 320 mapema jana kabla ya kurejeshwa tena huko huko kushiriki operesheni hii ya kuoko nafsi za watu wanaokisiwa kuwa takriban 3,000.BBC
No comments:
Post a Comment