Pages

August 1, 2015

MAFISADI WAHAHA KUMZUIA NAPE MTAMA

……………………………………………………………….
Ikiwa imebaki siku moja kufanyika kwa kura za maoni Ubunge
wa Jimbo la Mtama ,kumekuwa na michezo ya kumchafua kisiasa Katibu wa
NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye ni mmoja wa wagombea wenye
nguvu kubwa kwa jimbo la Mtama.
Huku hujuma hizo zikihusishwa na mikakati ya mafisadi
kumzuia Nape, ambaye amekuwa mwiba mkali sana kwa mafisadi kwa miaka
sasa, ametajwa aliyekuwa akitafuta kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia CCM ambaye jina lake lilikatwa katika hatua
za awali kuhusika na njama hizo chafu.
Taarifa zilizosambazwa jioni hii kwenye mitandao mbalimbali
zilidai Nape amehojiwa na Takukuru Lindi kwa Masaa matano wakati
haikuwa kweli.
Kamanda wa PCCB mkoa wa Lindi S. Chami amethibitisha kuwa
Nape Nnauye alikuwa ametoa pesa benki kwa ajili ya malipo ya mawakala na
si wajumbe kama ilivyovumishwa.
CORRECTION: After questioning, it turned out that the money Nape Nnauye
withdrew  was for agents, not delegates, Lindi  PCCB  boss S. Chami
clarifies Friday.”
Nape amesema anajua mafisadi wanahaha kumchafua hata kufikia hatua ya
kutumia baadhi ya watumishi wa serikali na mitandao ya kijamii lakini
hawatofanikiwa.
” Najua wanaogopa nikiingia bungeni itakuwa kiama chao, sasa wanahaha
kunizuia. Wametumia pesa na ghiliba za kila namna wanashindwa na
watashindwa vibaya kesho. Mungu mkubwa” alikaririwa Nape

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...