Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata
utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga yenye urefu wa
kilomita 60, hafla hiyo imefanyika jana Agosti 7 2015 mkoani
Lindi.Wengine pichani ni Balozi wa Kuwait Jassem Ibrahim Al
Najem,Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait, Abrahman Al- Hashim,Mkuu wa Mkoa wa
Pwan, Eng. Evarist Ndikilo, wengine kushoto ni Waziri wa ujenzi
Mhe.John Pombe Magufuli, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mkuu wa mkoa
wa Lindi Mhe.Mwantumu Mahiza.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazia Dkt.Jakaya Kikwete akiwa kwenye picha
ya pamoja na viongozi mbali mbali mara baada ya kufunguarasmi barabara
ya Ndundu - Somanga.
Rais
Kikwete akimshukuru Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait ,Abrahman Al Hashim
mara baada kuweka jiwe la msingi wakati wa sherehe fupi zilizofanyika
kwenye kijiji cha Marendego ,wakati wa ufunguzi wa barabara ya
Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa
kiwango cha lami.
Rais
wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa pamoja na mkewe
Salma Kikwete akimwagia maji mti wa kumbukumbu alioupanda baada ya
ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga mkoani Lindi.
Wafadhili
wa ujenzi wa barabara ya Ndundu-Somanga, Balozi wa Kuwait Jassem
Ibrahim Al Najim na Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait ,Abrahman Al Hashim
mara kwa pamoja wakishiriki kupanda mti wakati wa sherehe fupi
zilizofanyika kwenye kijiji cha Marendego ,wakati wa ufunguzi wa
barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na
imejengwa kwa kiwango cha lami.
Rais
Kikwete akiwasalimia na kuwaaga wananchi wa kijij cha Nangurukulu na
kumtambulisha Mgomea Urais kwa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli
alipokuwa akielekea mkoani Lindi.
Mgombea
Urais wa chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akijitambulisha
kwa wakazi wa mji wa Nangukurulu,mara baada ya sherehe fupi za ufunguzi
wa barabara ya Ndundu-Somanga kukamilika mkoani Lindi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na
Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mgombea mteule wa Urais wa chama cha
Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili katika kijiji cha
Marendengo Wilayani Kilwa mkoani Lindi kufungua barabara ya
Ndundu-Somanga yenye urefu wa kilometa 6.Barabara hiyo imejengwa na
Serili ya Tanzania kwa kushirikiana na Ufadhili wa Mfuko wa Kuwait
pamoja na mfuko wa OPEC .
Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akipokelewa na Mkuu
wa mkoa wa Lindi,Mh.Mwantumu Mahiza mara baada ya kuwasili katika
kijiji cha Marendengo Wilayani Kilwa mkoani Lindi kushiriki ufunguzi wa
barabara ya Ndundu-Somanga yenye urefu wa kilometa 6.Barabara hiyo
imejengwa na Serili ya Tanzania kwa kushirikiana na Ufadhili wa Mfuko wa
Kuwait pamoja na mfuko wa OPEC .
Waziri
wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya
Nje na ushirikiano wa Kimataifa,Mh.Bernad Membe mara baada ya kuwasilia
katika kijiji hicho Marendengo,ambapo
sherehe za uzinduzi wa barabara ya Ndundu-Somanga zilifanyika na mgeni
Rasmi alikuwa ni Rais Dkt Jakaya Kikwete.
Dkt
John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete,kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh Said Meck
Sadick akiwa sambama na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh.Mwantumu Mahiza.
Wananchi
kutoka kijiji cha Marendego na vijiji vyake wakishangilia jambo wakati
wa ufunguzi wa barabara ya Ndundu –Somanga yenye urefu wa kilometa
6,inayojengwa na Tanzania kwa kushirikiana na Ufadhili wa mfuk wa Kuwait
pamoja na Opec.Katika unziduzi huo viongozi mbalimbali wa chama na
serikal,viongozi wa dini pamoja na watu wengine walishiriki kushuhudia
tukio hilo adhimu hapa nchini.
Wananchi wakifuatilia tukio hilo
Dkt
John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi mbalimbali wa chama na
serikali wakati wa ufunguzi wa barabara hiyo ya Ndundu -Somanga yenye
urefu wa kilometa 60
Wananchi wakifurahia ufunguzi wa barabara hiyo iliyokuwa kero kubwa kwa wananchi wa Mtwara na Lindi
Waziri
wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe
akizungumza na Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli wakati wa sherehe
fupi za ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga iliyojengwa kwa kiwango
cha lami na yenye urefu wa kilometa 60 ,Somanga mkoani Lindi.
Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa,Mh Bernad Membe
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu wananchi waliojitokeza kushuhudia
ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga yenye urefu wa Kilomita 60
mkoani Lindi.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu wananchi waliojitokeza kushuhudia
ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga yenye urefu wa Kilomita 60
mkoani Lindi.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu wananchi waliojitokeza kushuhudia
ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga yenye urefu wa Kilomita 60
mkoani Lindi.
Waziri
wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wakati wa sherehe
fupi zilizofanyika kwenye kijiji cha Marendego kata ya Somanga za
ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa
kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi
wakati wa sherehe fupi ya ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani
Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.
No comments:
Post a Comment