Pages

August 29, 2015

Hukumu ya waandishi hawa baada ya kutangaza habari za uongo…


aljazera
Mahakama ya Misri imewahukumu waandishi watatu wa kituo cha runinga cha Al jazeerakwenda jela miaka mitatu.
Hukumu hiyo ilitolewa baada ya waandishi hao Mohamed Fahmy, Peter Greste na Baher Mohamed kupatikana na hatia ya kutangaza habari za uongo na kulisaidia kundi laMuslim Brotherhood ambalo kwa sasa linatambuliwa kama kundi la kigaidi.
Baher Mohamed pia alihukumiwa kifungo kingine cha miezi sita.
Hata hivyo mmoja wa waandishi hao Peter Greste, yuko nje ya nchi hiyo baada ya kutimuliwa kutoka nchini kwake tangu mwezi Ferbruari.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...