Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima aliyeshinda katika
kura za maoni za kutafuta wabunge wa viti maalum mkoa wa Arusha kupitia
jumuiya ya wazazi wa chama cha Mapinduzi ( CCM ).akizungumza katika
mkutano wa chama cha mapinduzi jana mtaa wa kati (CCM MKOA)wakati
wagombea 12 wa chama hicho walipofanya ziara ya kutembelea kila kata na
kujinadi kwa wananchi pamoja na wanachama wa chama hicho ambapo
aliwataka wananchi wasirubuniwe na kama walipewa rushwa na mgombea
yeyote wasimchague bali wamchague kiongozi sahihi wa kuleta mabadiliko
ya kimaendeleo katika jimbo la Arusha(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalimaambaye alishinda katika
kura za maoni za kutafuta wabunge wa viti maalum mkoa wa Arusha kupitia
jumuiya ya wazazi wa chama cha Mapinduzi ( CCM ). ambaye pia ni Afisa
masoko wa Triple "A",Mkurugenzi wa Phide entertainment akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Monaban yajijini Arusha,Philemon Mollel ambaye pia ni Mgombea Ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM katika ofisi za (CCM Mkoa) jijini Arusha jana
Katibu wa wazazi Mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau
akizungumza katika mkutano wa kuwanadi wagombea Ubunge kupitia chama
cha mapinduzi mtaa wa kati jijini Arusha ambapo aliwataka wapambe
wawagombea watulize mung'ari zao na kuacha tabia ya kukebihana huku
akisisitiza wananchi kuchagua kiongozi bora
Kada maarufu wa chama cha mapinduzi ambaye pia ni mfanyabiashara wa madini jijini Arusha Justine Nyari, anayeomba ridhaa ya ccm katika nafasi ya ubunge akiteta
jambo na Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima ambaye pia ni
Afisa masoko wa Triple "A" na Mkurugenzi wa Phide entertainment kabla ya
mkutano wao wa kujinadi kuanza
Mbunge
viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima ambaye pia ni Afisa masoko wa
Triple "A"na Mkurugenzi wa Phide entertainment akibadilishana mawazo na
wakili msomi Edimond Ngemela anayeomba ridhaa ya ccm katika nafasi ya ubunge
Mbunge
viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima ambaye pia ni Afisa masoko wa
Triple "A" na Mkurugenzi wa Phide entertainment akiwa katika picha ya
pamoja na watia nia nafasi ya Ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM
Mbunge
viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima ambaye pia ni Afisa masoko wa
Triple "A"na Mkurugenzi wa Phide entertainment, akisalimiana na mtia nia
nafasi ya Ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM Thomas Munisi ,ambapo Mwakitalima aliibuka
mshindi katika kura za maoni za kutafuta wabunge wa viti maalum mkoa wa
Arusha kupitia jumuiya ya wazazi wa chama cha Mapinduzi ( CCM ).
Mbunge
viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima ambaye pia ni Afisa masoko wa
Triple "A" akisalimiana na wadau ambao ni watia nia Ubunge na
Udiwani,kushoto ni Simba Salum anayeomba chama cha mapinduzi kumpitisha
kuwania nafasi ya udiwani mtaa wa kati bondeni na kulia wakili msomi
Edimond Ngemela anayeomba ridhaa ya ccm katika nafasi ya ubunge
No comments:
Post a Comment