Katibu
wa vijana umoja wa vijana UVCCM wilaya ya Arusha mjini Jamali Khimji
akimkabidhi fomu ya ubunge viti maalum Bi.Neema Kiusa(27)katika ofisi za
umoja huo jijini Arusha, ahaidi kuinua vijana kiuchumi endapo atapata
nafasi ya kuwa Mbunge wa vijana Mkoa wa Arusha(Habari Picha na Pamela
Mollel wa jamiiblog)
Neema
Kiusa(27) Mgombea ubunge viti maalumu kupitia chama cha Mapinduzi
ambaye pia ni mjumbe wa baraza la vijana wilaya ya Longido akionyesha
fomu aliyochukua leo.
Neema
Kiusa(27)ambaye ni mgombea ubunge viti maalumu kupitia chama cha
Mapinduzi akiwa na mumewe Andrea Shija, pia ni mama wa mtoto mmoja.
Neema Kiusa(27)Mgombea
ubunge viti maalumu kupitia chama cha Mapinduzi ambaye pia ni mjumbe
wa baraza la vijana wilaya ya Longido akitoka katika ofisi za umoja wa
vijana wa CCM mkoa wa Arusha baada ya kuchukua fomu.
Mgombea
ubunge kupita kundi la vijana (UVCCM) Neema Kiusa amechukua fomu
ya kuwania nafasi ya ubunge viti maalumu Mkoa wa Arusha,ambapo amesema
kuwa shauku yake kubwa ni kuwatumikia vijana kwa kutatua changamoto ya
ajira.
Neema
ambaye pia ni mjumbe wa baraza la Vijana Wilaya ya Longido alisema kuwa
ndoto yake ya kuwatumikia vijana ni ndoto yake ya muda mrefu sana hivyo
endapo atapata nafasi hiyo atashirikiana na vijana bega kwa bega kuleta
maendeleo katika Mkoa wa Arusha.
Pia
mgombea huyo alitoa shukrani kwa mume wake anayempa ushirikiano mkubwa
wa kufanikisha ndoto yake ya kutumikia vijana ambapo aliwataka wanaume
wengine kuonyesha ushirikiano kwa wake zao endapo wataonyesha nia ya
kuwania nafasi za uongozi.
Kwa
upande wake Katibu wa vijana UVCCM wilaya ya Arusha mjini Jamali Khimji
amewataka vijana wa chama cha mapinduzi kujitokeza kwa wingi kuchukua
fomu za nafasi za ubunge viti maalumu kundi la vijana katika mkoa wa
Arusha.
Khimji
alisema kuwa kijana anayetakiwa kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ni
kijana wa kwanzia umri wa miaka 21-30 na awe ametimiza vigezo vya chama
hicho.
No comments:
Post a Comment