Katibu msaidizi wa CCM Iringa mjini akipokea fomu ya balozi Augustino Mahiga anayeomba kugombea ubunge jimbo la Iringa mjini. |
Balozi Mahiga akirejesha fomu za ubunge jimbo la Iringa mjini .
Balozi Mahiga akiweka sahihi kitabu cha wageni .
Na Matukiodaima BLOG
ALIYEKUWA
mmoja kati ya wagombea zaidi ya 40 wa wagombea wa nafasi ya urais
Balozi mstaafu Augustino Mahiga amejitokeza kuchukua na kurejesha fomu
wa ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha mapinduzi (CCM)
huku akijihakikishia kuwa ndie anayestahili kumpokea ubunge
aliyemaliza muda wake mchungaji Peter Msigwa (Chadema)
Balozi
Mahiga alieleza kuwa yeye baada ya kustaafu nafasi ya ubalozi moja
kati ya ndoto yake ni kuendelea kuwatumikia wananchi kwa ngazi ya
ubunge ama udiwani kazi ambayo anaamini ataifanya kwa uadilifu mkubwa
kama alivyofanya katika nafasi ya ubalozi wa Tanzania katika nchi mbali
mbali .
Akizungumza na wanahabari baada ya kurejesha fomu hiyo ya ubunge katika
jimbo la Iringa mjini Balozi Mahiga alisema kuwa sababu kubwa ya
chama kupoteza umaarufu wake ni makundi na rushwa kwa baadhi ya
wagombea na kuwa ni vema wana CCM kuvunja makundi ya waliokuwa
wagombea wa nafasi za urais ili kuepuka kuingiza makundi hayo katika
nafasi za ubunge na udiwani .
Kwani
alisema kwa upande wake haungi mkono baadhi ya wana CCM kuendesha
makundi na kuwa ndoto yake ni kuwatumikia wananchi hivyo baada ya
safari yake ya kutaka kuomba ridhaa ya wana CCM kugombea Urais
kushindikana kwa sasa atamuunga mkono kwa nguvu zote mgombea wa CCM Dr
John Mkagufuli na kuwa yeye ameamua kugombea ubunge japo alikuwa
tayari hata kuwatumikia wananchi kwa nafasi yoyote ukiwemo udiwani .
Alisema
kipaumbele chake kikubwa ni kusimamia na kutekeleza kwa makini
ilani ya CCM na kuwa tofauti yake na aliyekuwa mbunge wa jimbo la
Iringa mjini kupitia chadema ni moja kwani yeye ni mtendaji kwa vitendo
zaidi na sio maneno pekee .
Kwani
alisema kawaida ubunge ni kupokezana na kuwa Chadema walipokea
jimbo hilo kutoka mikononi mwa CCM hivyo lazima Chadema kupokelewa
jimbo na CCM na mtu pekee anayestahili kuwatumikia wana Iringa ni yeye
pekee.
Alisema
Iringa kama kitovu cha utalii kwa mikoa ya nyanda za juu kusini
anaamini iwapo chama kitamteua na kuwa mbunge wa jimbo hilo
atahakikisha sekta hiyo inawanufaisha wananchi wake zaidi ikiwa ni
pamoja na kuboresha makazi na nyumba kwa kuweka mkakati kamili wa
kufanya hivyo.
Aidha
alisema kuwa dhana ya kutumia pesa ili kupata nafasi ya uongozi
kama ilivyokuwa kwa wagombea Urais inaweza kuendeleza kugawa CCM
na kuwa utaratibu wa CCM wa kuwatembeza wagombea katika chombo
kimoja cha usafiri utasaidia kupunguza makundi ndani ya chama
hicho na kuwaonya watia nia wenzake kuheshimu matokeo baada ya
mgombea kuteuliwa na kuungana nae ili kumnadi yule aliyepitishwa na
chama .
Katika
jimbo la Iringa mjini hadi leo majira ya saa 10 juioni jumla ya
wagombea 13 waliochukua fomu waliweza kurejesha fomu .
No comments:
Post a Comment