Pages

June 30, 2015

TANAPA MEDIA AWARDS 2014 YAFANA JIJINI MWANZA

Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akimkabidhi tuzo maalum ya heshima Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali  Mirisho Sarakikya akiwa na mkewe kwa kupanda mlima Kilimanjaro mara 38, Jenerali Sarakikya pia  amepewa Kadi maalum ya kuingia mbuga zozote za TANAPA bure yeye pamoja na familia yake, lakini katika hatua nyingine  atalipiwa gharama zote za kushiriki mkutano wa masuala ya utalii kuhusu milima mirefu zaidi duniani  yeye pamoja na mke wake huko nchini Marekani, Katika mkutano huo Jenerari Sarakikya anatarajiwa kutoa  mada kuhusu mlima Kilimanjaro.
Jenerali Mirisho Sarakikya  amekabidhiwa tuzo hiyo katika hafla ya utoaji wa tuzo za TANAPA za waandishi wa habari za utalii iliyofanyika kwenye hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo  ambapo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali  wamepewa tuzo hizo. Katika picha kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi za mbuga za Taifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akizungumza katika hafla ya utoaji wa tuzo za TANAPA za waandishi wa habari kwenye hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza usiku wa kuamkia .
Meneja  wa Mawasiliano TANAPA Bw. Pascal Shelutete akitoa utaratibu wa utoaji wa tuzo hizo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo  Festo Sikagonamo mwandishi bora wa  habari za utalii vipindi vya redio katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni  Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Magessa Maggesa  mwandishi bora wa habari za utalii kwa vipindi vya Televisheni kutoka Stars TV katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Jimmy Mengere kutoka Chanel Ten  Morogoro, mwandishi bora wa habari za utalii kwa habari za Utalii aliyeandika kuhusu wanyama wanavyouwawa kwa ajali katika mbuga ya Mikumi.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Kasilda Mlimila Mwandishi bora wa habari za utalii za Televisheni kutoka Star TV Morogoro  kwa kuandika kukauka kwa mto Ruaha Mkuu , kulia ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni  Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Jackson Kalindimya Mwandishi bora wa habari za Utalii Magazeti  katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Humphrey Mganga  mwandishi bora wa habari za utalii katika magazeti katikati ni  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza,Mh Baraka Konisaga

 Mwenyekiti wa jopo la Majaji TANAPA Media  Awards,Dkt.Ayub Rioba.


 Katibu Mkuu wa  Maliasili na Utalii,Dk Adelhim Meru


Mwandishi wa gazeti la Mwananchi mkoani Arusha,Mussa Juma(kulia)akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Tsh.1.5 milioni.







Mwandishi wa Star Tv mkoani Morogoro ,Kasilida Mlimila akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Tsh.2 milioni baada ya kushinda tuzo ya uandishi bora ya utalii wa ndani ,Hifadhi ya Taifa Udzungwa.


Mwandishi wa gazeti la Mwananchi mkoani Kagera ,Phiniasi Bashaya akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Tsh.1.5 milioni kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu .






Waziri wa Maliasili na Utalii ,Mh.Lazaro Nyarandu



Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu katikati, Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi wa TANAPA na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Mwanza kwenye hoteli ya Gold Crest.






 Mwenyekiti wa jopo la Majaji TANAPA MEDIA AWARDS,Dkt.Ayub Rioba

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...