Pages

June 3, 2015

SERIKALI IWEKE KIPAUMBELE KWENYE LISHE

Katibu Mtendaji wa Shirika lisilokua la kiserikali la ANGONET lenye makao makuu  jijini Arusha ,Peter Bayo (kushoto)  akizungumza na waandishi wa habari  juu ya masuala ya lishe na kuitaka serikali iweke vipaumbele katika lishe ili kutokomeza matatizo ya udumavu na utapiamlo,Katikati ni Mratibu wa Angonet ,Petro Ahham na Jovitha Mlay mwanachama wa shirika hilo.
Mratibu wa Angonet ,Petro Ahham akifafanua juu ya Mkakati wa Lishe wa taifa wa July  2011/12 hadi Juni 2015/16 kwa waandishi wa Habari  katika mkutano na waandishi juu ya hali ya lishe nchini na namna ya kuhamasisha lishe ili kuondokana na udumavu na utapiamlo,Kulia ni Katibu Mtendaji wa shirika lisilokuwa la kiserikali (ANGONET) ,Peter Bayo.Picha na Ferdinand Shayo  


Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Serikali imetakiwa kuweka vipaumbele katika masuala ya lishe ili kutokomeza matatizo ya udumavu na utapiamlo yanayosababishwa na lishe duni hivyo kuathiri maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

Katibu Mtendaji wa shirika lisilokuwa la kiserikali (ANGONET) ,Petter Bayo amesema kuwa kutokana na hali mbaya ya lishe nchini na kuongezeka kwa udumavu wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano 5 hadi kufikia asilimia 42% ya watoto hao kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2012.

Bayo alisema hayo jana akizungumza na Waandishi wa habari amesema   kuwa iwapo hatua za makusudi hazitachukuliwa athari zitakua kubwa katika shughuli za uzalishaji kutokana na lishe duni na pia kuathiri Nyanja za elimu na sekta mbali mbali kuwa  hayo jana akizungumza na Waandishi wa habari.

“Lishe ni kiini cha maendeleo ya jamii yoyote ile na nchi yoyote ile ni vyema serikali ikatilia mkazo suala la lishe kwani ni kichocheo muhimu cha maendeleo kwa kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi hasa waishio vijijini” Alisema Bayo

Mratibu wa Angonet ,Petro Ahham alisema kuwa Serikali inapaswa kutupia macho suala la upatikanaji wa chakula na kuangalia uhaba wa chakula unaoweza kusababisha watu kufa kwa kukosa chakula.

Ahham anaeleza kuwa ukosefu wa madini chuma kwa watoto umekua ukisababisha ugonjwa wa Anemia unaowapelekea watoto kusinzia wakiwa mashuleni hata kuchangia kushuka kwa kiwango cha ufaulu  kutokana na Lishe duni.

Mwanachama wa Angonet ,Jovitha Mlay anaeleza kuwa shirika hilo kwa sasa linashirikiana Umoja wa mashirika yanayojihusisha na masuala ya  lishe Tanzania (PANITA) katika kutoa elimu juu ya lishe na kufanya uhamasishaji mashuleni na katika makundi mbalimbali ya jamii husasan kwenye Kanda ya Kaskazini,mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Manyara.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...